Thursday, June 25, 2015

UMEISOMA HII: Waandikishaji BVR wafungiwa kituoni

Geita. Kazi ya uandikishaji wapigakura imezidi kukumbwa na matatizo baada ya wananchi kuwafgungia waandikishaji ndani ya kituo kutokana na kupata taarifa kuwa muda uliopangwa kwa ajili ya mitaa ya Buhalahala, Kisesa na Moringe umekwisha, huku wakiwa hawajapata nafasi ya kusajiliwa.
Wakati vurugu hizo zikitokea, wananchi wa kata nne za wilayani Bukombe wanahofia kukosa nafasi ya kuandikishwa kutokana na maeneo yao kutoingizwa kwenye mfumo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), huku watu watatu, wakiwamo watoto wawili wilayani Hanang wakikamatwa kutokana na kujiandikisha mara mbili huku wakiwa hawajafikia umri unaotakiwa.
Tukio la Geita limetokea siku chache baada ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwataka wananchi mkoani Kilimanjaro kutoruhusu mashine zinazotumika kuandikishia wapigakura kwa njia ya kielektroniki (BVR) kuondolewa vituoni endapo kuna watu ambao hawajaandikishwa.
Uandikishaji mkoani Geita ulianza Juni 17, mwaka huu kwa kata tatu za Buhalahala, Mwatulole na Kalangalala na muda uliopangwa kumalizika ni juzi. Hali ilikuwa mbaya kwenye kata hizo baada ya wananchi kukaa vituoni hadi usiku wakisubiri kuandikishwa, na walipopata taarifa kuwa kazi hiyo haitaendelea kwa kuwa siku zilizopangwa zimemalizika, walichukua uamuzi huo wa kuzuia waandikishaji hadi watakapoandikisha wote waliokuwa wamesalia.
“Nimekuja hapa nina siku ya tano leo (juzi). Kila nikija sipati nafasi ya kuandikishwa wengine wanakesha vituoni siku ya tano, lakini hawajaandikishwa na leo ndiyo mwisho,” alilalamika mkazi wa Mwatulole, Marwa Ernest.
Mkazi mwingine, Neema Charles alisema:“Mwandikishaji anatuambia macho hayaoni, kwa hiyo sisi tufanyeje, tunataka kitambulisho kwani ndiyo cha msingi mwaka huu.”
Wananchi hao ambao walionekana kuwa na jazba, huku wakitishia kuchoma mashine kama wasingeandikishwa, walidai kuwa shughuli hiyo imetawaliwa na rushwa.
Hali hiyo ilikikumba kituo cha Shule ya Sekondari ya Kalangalala, ambako hadi saa 1:30 usiku mwandishi alishuhudia zaidi ya wananchi 200 wakiwa kituoni wengine wakipigana na kusukumana kila mmoja akitaka kuandikishwa.
“Hapa muda unaisha na leo (juzi) ndiyo mwisho, hatujui hatima yetu, wananchi wengi hatujaandikishwa, tumeshaomba tuongezewe mashine lakini hatusikilizwi zaidi tunashuhudia wenye fedha ndiyo wanaandikishwa,” alisema mkazi wa Kisesa, Mariana Peter.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Hellen Kahindi alikiri kuwapo kwa vurugu hizo na kwamba walikosea kuweka vituo pembezoni mwa mji, jambo lililosababisha wananchi wa mjini kukimbilia maeneo hayo wakihofia kutoandikishwa.
Alisema vurugu hizo zilisababisha magari mawili ya Serikali kuvunjwa vioo, huku waandikishaji wakiponea chupuchupu kutokana na kuwapo na vurugu kubwa eneo la kutokea hadi polisi walipoingilia kati.
“Tunashukuru hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa waandikishaji na vifaa, lakini tumejipanga kwa zoezi hili jipya ili matatizo hayo yasijitokeze kwani tumeongeza wino na kwenye mashine,” alisema Kahindi.

Wanafunzi Nchini Marekani wavumbua Kondomu inayotambua Maambukizi ya Zinaa

Wanafunzi katika shule ya  Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayobadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
 
Kondomu hiyo iliyopewa jina la S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono huku ikiwa na uwezo wa kubadili rangi tofauti kulingana na bakteria waliopo.
 
Miongoni mwa wafumbuzi waliofanya uvumbuzi huu ni Daanyaal Ali (14), Muaz Nawaz (13) na Chirag Shah (14), ambapo kufuatia ufumbuzi huo tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ”the TeenTech” sambamba na kutunukiwa pauni elfu moja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.
 
Akifafanua juu ya uvumbuzi huo, mmoja wa wanafunzi hao Daanyaal Ali amesema kuwa  “Tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini kwa ajili ya kizazi kijacho”.
 
Aliongeza kuwa “Swala la usalama wa mpenzi ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaumbele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia”
 
Kwa upande wake Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Maggie Philbin alisema kuwa ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa lengo la kuboresha maisha ya mwanadamu.
Mpekuzi blog