Saturday, July 11, 2015

Live Dodoma: Polisi Watumia Mabomu Kuwatawanya Wafuasi wa Lowassa Waliokuwa Wakiandamana


Wapambe wa Mbunge  wa Monduli Edward Lowassa  hivisasa wanafanya maandamano makubwa nje ya ofisi za CCM hapa makao makuu ya CCM wakipinga Mbunge huyo kuchujwa katika tano bora.

Wapambe hao wanaimba nyimbo mbalimbali za kukiponda chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa chama hicho sio cha kindugu na  pia sio cha kifalme.

Kwa namna nyingine  hali si shwari hapa mkoani Dodoma ambapo sintofahamu imetawala kuhusiana na Edward Lowassa kukatwa.

Bado haijulikana nini hatma ya kikao kinachoendelea hivisasa kwa kuwa wa wajumbe wengi wa napinga Lowassa kuchujwa.
Baishara zasimama,makao makuu Dodoma.
Baadhi ya wapambe wa Lowassa wakipinga Kamati kuu kumchuja Lowassa.
Barabara zafungwa Polisi watanda kila kona kudhibiti usalama dhidi ya waandamanaji.
Wapambe wa Loawssa wakipinga kukatwa tano bora

No comments :

Post a Comment