Wapiganaji wa kundi la Alshabaab wamevamia hoteli mbili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu .
Mwandishi wa BBC katika mji huo anasema kuwa oparesheni ya usalama katika hoteli ya Weyhliya iliopo karibu na bunge imekamilika.
Amesema kuwa takriban watu watano wameuawa pamoja na wapiganaji watatu.
Amesema kuwa milio ya risasi bado inasikika katika hoteli ya Siyaad karibu na makao ya rais.
Kundi hilo pia lilirusha kombora katika makao makuu ya umoja wa Afrika mjini humo.
Source: BBC
No comments :
Post a Comment