Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kumpata mpinzani wake Mwalimu wa Kitengo cha Kompyuta toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Anthony Kalokola kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika
Jimbo la Ukonga.
Jimbo hilo limekuwa wazi tangu Juni 2, mwaka huu alipofariki Mbunge wa Jimbo hilo, Eugen Mwaiposa, nyumbani kwake mjini Dodoma, hivyo wakazi wengi walimpatia nafasi Meya huyo kutokuwa na mpinzani.
Wakazi wa jimbo hilo walikuwa kimya kwa kipindi fulani bila kujihusisha na shughuli za kisiasa, lakini imewashangaza kipindi hiki watu kujitokeza kutimiza wajibu wao kikatiba kwa kugombea nafasi mbalimbali, ikiwamo ubunge na udiwani.
Kalokola ambaye ni mmoja wa wagombea alisema yeye ameamua kuchukua na kurejesha fomu ili kugombea nafasi ya ubunge , hivyo hawezi kuzungumza chochote bali Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itawapatia nafasi ya kuzungumza chochote, lakini kiongozi yeyote anapaswa kuwa mbunifu.
No comments :
Post a Comment