Monday, July 20, 2015

MAMBO KUMI UNAVYOTAKIWA KUYAACHA MARA MOJA

                       
Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kukufanya ukose raha na kupata "stress". Hivi ni vitu 11 ambavyo unatakiwa kuviacha ili kurahisisha maisha. Anza leo kuviacha kwani kuendelea kuvifanya vitu hivi hakutakusaidia chochote .
Vitu kumi ambavyo unatakiwa kuviacha mara moja ni hivi vifuatavyo;

1. Achana na tabia ya kukataa mabadiliko
Mabadiliko ni kitu muhimu sana katika maisha, kwani mabadiliko hufanya maisha
kuwa ya furaha na amani. Unapokataa mabadiliko unazuia nafasi ya upendo na vitu vingine vizuri kuja katika maisha yako. Mara nyingi mabadiliko hufanyika pale unapotaka kufikia malengo fulani. Vile vile mabadiliko hufanyika ili kukupa nafasi ya kuendeleza career yako. Kwahiyo achana na tabia ya kukataa mabadiliko kwani unauwezo wa kuyafanya mabadiliko yatakayokupa manufaa katika maisha yako.


2. Usifikiri kwamba unaweza ku-control kila kitu katika maisha yako.
Ni muhimu sana kufahamu mipaka ya vitu ambavyo unauwezo wa kuvifanya au kuvi-control. Ni rahisi sana kufanya mabadiliko katika maisha yako, fikra zako, matendo yako lakini huwezi kuwabadilisha wengine. Huwezi badilisha hali ya hewa, au fikra na imani za ndani za wazazi wako. Mara nyingi ukitumia nguvu kubwa kubadilisha tabia za watu utaishia kujiumiza. Cha muhimu ni kuyapa kipaumbele maisha yako na ku-deal nayo zaidi na vitu vingine vitafuata.


3. Usipende sana kutafuta sababu au visababu
Unaposhindwa kufanya jambo, kutafuta sababu ya kushindwa siyo jambo la msingi. Kila mtu anaweza akaona au kuhisi kwamba unatafuta sababu ya kuongezewa muda au sababu ya kutokufanya hilo jambo. Kutafuta sababu au visababu ni kupoteza muda. Amua jambo moja kufanya au kutokufanya jambo, then maisha yaendelee.



4. Usipende kulaumu wengine.

Hakuna ambaye anaweza kukuzuia usifanye au usipate kitu chochote katika aisha yako. Jukumu la ko kuyaendesha maisha yako mwenyewe kwa asilimia mia. Hakuna mwingine ambaye anataweka fikra katika kichwa chako au vikwazo vyako katika maisha yako. Hakikisha watu wanaokuzunguka ni wale wanaoamini ndoto zako.


5. Usipende kulalamika.

Hichi ni kitu kingine ambacho kinaweza kukupotezea muda. Unapokuwa unalalama mara nyingi fikra zako zinakuwa zimejikita kwenye mambo ambayo huyapendi au hutaki yatokee. Ni muhimu kujua kwamba mara nyingi jambo au mambo ambayo tunayafikiria ndiyo hayo ambayo hutokea au kujitokeza. Fikra zako zinaweza kukuksaidia kufanikisha au kuleta jambo ambalo unalitaka. Cha msingi ni kuelekeza akili zetu katika fikra nzuri za mafanikio na zinazojenga badala ya kuzielekeza kwenye fikra ambazo hazitusaidia.



6. Achana na dharau na kuwakashifu.

Mara nyingi dharau na kashfa hutokea pale unapojiamini kupita kiasi au kuamini kwamba huwezi kukosea. 

Kama unatabia ya kutafuta makosa hata kwenye vitu vidogo kwa watu unaokutana nao ni bora kuacha kwani haitakusaidia katika maisha yako. Tabia ya kudharau na kukashifu mara nyingi ni tabia ambayo inaweza kumvunja mtu moyo hivyo ni bora mtu uachane nayo, ubadilike na kuishi maisha ya kuwapa watu moyo na nguvu.
                                    


7. Usijiombee mabaya.
Kuna watu ambao huwa wanatabia ya kujiona kwamba wameshashindwa katika maisha yao. Mara nyingi maono yako ndiyo hujenda maisha yako. Kwahiyo kama unafikiria umeshindwa katika maisha ujue kweli utashindwa. Unatakiwa mara kwa mara uwe unafikiria njia za kujikomboa, badala ya kufikiria jinsi gani maisha yamekushinda. Ili kuwa na furaha ni jambo jema kujipa moyo kwamba kila kitu kitakua sawa na maisha yataenda jinsi unavyotaka.

                                     




8. Siyo lazima kuwa sahihi kila wakati 


Ni matatizo makubwa kufikiria na kuonyesha kwa watu ni jinsi gani upo sahihi au hauna makosa kwani hautapita muda mrefu utakosa cha kuwaonyesha. Hakuna mtu anayependa kuwa chini au kuona jinsi gani upo sahihi au ni jinsi gani wanakosea au wanamakosa. Fikra za kutaka kuwa sahihi kila wakati zitakuharibia maisha yako na mahusiano yako na watu wengine au wafanya kazi wenzako.



9. Maisha yako yaliyopita yasiyaathiri maisha yako ya sasa
Wengi wetu tunatabia yakutumia uzoefu wetu wa maisha ya nyuma au yaliyopita ili kuyatengeneza maisha ya sasa. Hilo siyo sawa kwani maisha yetu hujengwa na wakati tulionao  na wakati ujao na siyo wakati uliopita. Kama maisha yako yanatawaliwa na mawazo yaliyopita na kukufanya ujisikie kujuta au kukasirishwa na maisha yako ya sasa ujue unakosea. Jaribu kuyapenda maisha yako ya sasa kwa kuachana na mawazo au fikra za maisha yaliyopita.
                                 


10. Usiishi maisha ya kuwaridhisha wengine
Amini kwamba maisha yako yapo tofauti. Hakuna mtu mwingine katika dunia hii ambaye anaona na kufikiria kama jinsi wewe unavyoona na kufikiria, kwahiyo kuishi maisha ya kuwaridhisha wengine ni kupoteza muda.

Kunawatu ambao huishi maisha yao katika staili ambayo inalengo la kuwaridhisha wengine, au kulazimisha kuishi maisha ya kuigiza. Nafikiri tunawafahu watu ambao wapo radhi ata kuazima magari, nguo  au hata nyumba ili wawaonyeshe wengine kwamba wapo vizuri. iwapo utaachana na maisha ya kuigiza maisha yako yatakuwa ya amani na furaha. Na katika dunia hii hakuna kitu kizuri kama kujikubali na kuyakubali maisha yako. Utajisikia mwenye amani na upendo iwapo utajiamini na utaachana na fikra za kuanguka aukushindwa maisha.
                                   


No comments :

Post a Comment