Tuesday, September 8, 2015

SABABU TANO KWANINI UNATAKIWA KULA NDIZI


Wewe ni mpenzi wa ndizi? Je, unakula ndizi ngapi kwa siku, week, mwezi na mwaka? Je, unafahamu umuhimu wa ndizi kwenye afya yako?
Kutokana na mambo ya lishe kushika kasi hapa nchini kuna watu wengi wana hamu sana ya kufanamu masuala ya lishe. Kunahabari nyingi na ushauri mwingi ambao watu wanaupata kuhusiana na mambo ya lishe na matumizi ya ndizi. Zingine zinapotosha zingine ni za kweli.

Kuna baadhi ya washauri wa mambo ya lishe wamefikia hatua hata ya kushauri watu wasitumie ndizi kwenye mlo wao kwa sababu ya habari kwamba ndizi inachangia katika kuongezeka kwa uzito (weight gain).
Hizi ni sababu tano kubwa tano ambazo za kwanini unapaswa kula ndizi na kuachana na habari zilizozagaa mtaani.

1. Ndizi hazitakufanya uwe mnene
Hiyo ni kweli kabisa. Ndizi ni rafiki 'wa-diet'. Ndizi moja ndogo ya kawaida ina uwezo wa kukupatia nguvu kiasi cha calori 110, gramu 30 za wanga na gramu 3 za nyuzi nyuzi (fiber). Ndizi vilevile inakupatia aina za wanga isiyomengenywa kwa uraisi (resistant starch) na kukufanya ujisikie kushiba kwa muda mrefu. Hii itakusaidia wewe unayependa kupungua uzito kupunguza kiasi cha chakula utakachokula kutokana na kujisikia kushiba. "Chamuhimu hapa kufahamu ni kwamba haiitajiki wewe kushinda njaa ili kuoungua unene au uzito."
2. Ndizi husaidia kupunguza pressure ya damu
Ndizi zina kiwango kikubwa cha madini ya potassium ( kiasi cha gramu 422 kwa ndizi ndogo) ambayo husaidia katika mzunguko wa damu na kupunguza uwezekano wa kupata pressure na matatizo ya moyo.
3. Ndizi ni chanzo kizuri cha vitamin C
Wengi ukizungumzia Vitamini C fikra zao huenda zaidi kwenye matunda machachu kama machungwa na malimao na kwenye matunda jamii ya zabibu na kusahau kuwa hata ndizi ni chanzo kizuri pia cha vitamin C. Ndizi ndogo ina uwezo wa kuupatia mwili asilimia 17 ya kiwango cha vitamin C kinachotakiwa na mwili kwa siku. Vitamin C ni muhimu katika kinga ya mwili na kuimarisha fizi na ngozi.
4. Ndizi ina uwezo wa kukupatia nguvu kwa haraka (energy boost)
Kama unahisi kuishiwa nguvu au unahitaji nguvu kwa haraka, unashauriwa kupata ndizi. Ndizi itakusaidia katika kupata nguvu na nyuzi nyuzi ambazo zinasaidia katika mmeng'enyo wa chakula.
5. Ndizi inasaidia kuondoa njaa.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Smell and Taste Treatment and Research Foundation iliyopo Chicago-Marekani, iwapo utakinusa chakula wakati unanjaa inaweza ikaufanya ubongo wako uhisi kwamba umekula hicho chakula moja ya vyakula vinavyoweza kukufanya uhisi hivyo ukikinusa ni ndizi. "Nafikiri tunafahamu kesi za wapishi kushiba jikoni sababu ya harufu". 
Hitimisho.
Siyo kila aina ya ushauri unaweza kukuaidia mara unapoufanyia kazi. Kilichoandikwa kwenye habari hii ni uchunguzi wa kitaalamu ambao ndiyo umekuja na haya majibu. Kama bado unahisi kwamba huwezi kupungua uzito ukila ndizi, basi jaribu kuinusa wakati unanjaa inaweza kukusaidia.

No comments :

Post a Comment