Saturday, June 27, 2015

UMUHIMU WA NYWELE KICHWANI

Na mchambuzi wetu.

 Mitindo ya nywele ni kati ya vitu vinavyotumika katika kumfanya mtu awe na muonekano mzuri na urembo. Wakati mwingine mitindo ya nywele huhusianishwa na utamaduni kama vile "Masai Style" au umarufu nafikiri unaifahamu "Baloteli style" .




 
 
 
 
 Maranyingi mitindo ya nywele hubadilishwa ili kumpa mtu muonekano mpya au kumfanya mtu aonekane wa kisasa zaidi kwa wakati huo. Nadhani unafahamu vizuri kuhusu mitindo ya nywele inayokua maarufu kipindi Fulani na kupotea.
 Niwangapi mnafahamu kwamba nywele ni Chanzo kikubwa cha Nguvu kwa binadamu? Nikiongelea nguvu namanisha nguvu za kila aina kuanzia misuli yetu hadi nguvu ya kufanya vitu kimiujiza au wazungu wanasema "SPIRITUAL POWERS". Kwahiyo basi nywele zinaumuhimu sana kwetu zaidi ya kutupatia muonekano mzuri.
Katika dunia hii, binadamu ndicho kiumbe pekee ambacho nywele zinakua "GROW" kichwani pale tu ukuaji unapoanza. Na iwapo nywele hizo zikiachwa bila kukatwa hukua kwa kiwango fulani kabla ya kuafikia kikomo. Urefu huo huo hutofautiana kulingana na mtu na mtu. Kwa mujibu wa utamaduni wa yoga"YOGIC TRADITION", Nywele ni zawadi "wonderful gift of the nature" ambayo husaidia kuongeza nguvu ya ndani ya mwili ambayo kila mtu anayo " kundalin energy"

 Picture
 
 Iwapo utaacha nywele zako zikuwe mpaka mwisho na kujiviringisha kwenye kichwa nguvu ya Uhai " Life force" itashuka toka kichwani kwako mpaka chini ya uti wako wa mgongo. Jinsi nguvu hizi zinavyoshuka chini ya uti wako wa mgongo ndivyo ambavyo uwezo wako wa kujibalance unavyozidi. Tuachane na mambo ya YOGA, na tujiulize je ni vipi na kwanini nywele zilianza kukatwa?



.

Ni lini na kwanini nywele zilianza kukatwa?

Picture
Historia inaonyesha kwamba miaka mingi sana iliyopita naongelea karne zilizopita, watu kutoka makabila na tamaduni mbalimbali walikua hawakati nywele. Nafikiri hili lipo wazi, angalia vizuri kwenye biblia na kuruhani au historian ya watakatifu na mitume na ma generous wa zamani na wasasa. Lakini watu hao wa zamani walikua wanakata nywele zao tu kwa lazima kama alama ya utumwa katika kipindi cha kukamatwa na utumwa wao. Hii ni kwa sababu kwa kipindi hicho wakamataji walielewa kwamba kulikua na aina fulani ya nguvu halisia ambayo ingepungua na kuzidhibitiwa iwapo nywele hizo zingekatwa .
 

Picture
Kwa mujibu wa historia ya watu wa China, mifupa ya sehemu ya mbele ya kichwa hupitisha mwanga kwenda kwenye glands za uti wa mgongo. Kupita huko kwa mwanga husaidia kuweka balance kati ya glandi za Thyroid na Pineal zilizopo kwenye uti wa mgongo. Hii husaidia ufanyaji mzuri wa kazi ya ubongo na ambayo mwisho wa siku husaidia katika kubalance homoni ya thyroxine na homoni za uzazi (sexual hormone). Kutokana na hilo China ilipotawaliwa na Mfalme Genghis Khan alikua akifahamu uwezo mkubwa wa akili ya watu wa China kutokana na nywele zao hivyo akawa anawalazimisha wanawake wote kukata mtindo wa nywele kama wa mdada hapo kushoto kwenye picha. Na ni mtindo ambao mpaka leo hii watu wanautumia bila kufaham origin yake.
.

Baada ya maka kupita ufahamu wa umuhimu wa nywele ulipotea. Ukataji wa nywele ukawa ni kitu maarufu sana, hali iliyosababisha kuvumbuliwa kwa mitindo mbalimbali ya nywele.
 
Sayansi inasemaje?
Picture
 
Nywele zinapokua kwenye kichwa na kufikia ukomo wake "maximum length" madini ya calcium, phosphorous na vitamin D hutengenezwa kwa wingi. Vitu hivi huingia kwenye mfumo wa mwili "Lymphatic fluid" na kwenye uti wa mgongo kupitia mirija iliyopo kwenye sehem ubongo. Kitendo hichi husababisha ukuaji mzuri kumbukumbu, nguvu ya mwili, stamina na utulivu.
 
Vilevile nywele hufanya kazi kama antenna ambayo husaidia kupitisha miale ya jua "sun energy" kwenda sehem ya mbele ya ubongo inayohusiana na kuona na kutafakari.

Iwapo umeamua kukata nywele zako, hautapoteza virutubisho peke yake bali utapoteza uwezo na nguvu zako, hivyo mwili wako utaanza kufanya kazi ya ziada ya kukuza upya nywele zako zilizopotea. Inaweza chukua miaka mitatu kutoka unapokata nywele zako mpaka zinapofikia ukomo wake.
Embu linganisha uwezo wako wa kutafakari na wa mke wako au girlfriend wako, mnalingana au kunakitu amekuzidi. Hakuna mchawi zaidi ya nywele zake ndefu asizozikata.


Nguvu ya nywele kwenye mwili

  • Nywele mbichi

Nywele zikiwa mbichi lazima zikaushwe ili kuepusha kuumwa na kichwa, vilevile unapoacha nywele zako mbichi husababisha kukatika katika. Uamuzi mzuri ni kukaa kwenye jua na kuacha nywele zako zikauke badala ya kukimbilia hair driers. Ukikaa kwenye jua nywele zitasaidia mwili wako kupata vitamin D.
Osha nywele zako mara unapopoteza mudi au ku-pata stress, hii itasaidia kutuliza stress na mood yako na kukurudisha katika ubora wako. Hii ndiyo maana huko India kuna utamaduni wa kuosha vichwa mara baada ya kutoka kwenye misiba. Umeipata hiyo?
  • Kuchana nywele kwa chanuo la mti/ mbao.

Picture
Miaka ya nyuma mama zetu na dada zetu au hata wazee wetu walikua wanachana nywele zao kwa kutumia chanuo la mti. Je, unafahamu njia hii ina umuhimu gani?
 
Ukichana nywele zako kwa chanuo la mti atleast mara mbili kwa siku inasaidia sana kuboresha mzunguko wa damu kichwani na kuisisimua. Ni option nzuri zaidi kutumia chanuo la mti badala ya kutumia chanuo la plastiki.
  Unapochana nywele zako kutokea mbele kwenda nyuma, nyuma kwenda mbele na kushoto kwenda kulia kwa mara kadhaa husaidia kupata msisimko na burudani. Kama ulikua umechoka hii ndiyo njia rahisi ya kuto uchovu.

Vilevile uchanaji huo wa nywele atleast mara mbili kwa siku huweza kuwasaidia wanawake kupata mzunguko mzuri wa hedhi, kuona vizuri na kuwa na mvuto na mchangavu wakati wote.  Kwahiyo kama wewe ni mwanamke achana na mambo ya mawigi na wivings.



 

Itaendelea...

No comments :

Post a Comment