Watu kadhaa wanao daiwa kuwa ni majambazi jana
walivamia Benki ya NMB tawi la Mkuranga mkoani Pwani na kupora fedha kisha
kumuua askari mmoja na kutokmea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafary Mohamed
alithibitisha jana jioni kupata taarifa za tukio hilo.
“Taarifa hizo nimezipata kuwa watu hao wanaodhaniwa
majambazi wamevamia Benki ya NMB, Mkuranga na kupora fedha ambazo kiasi chake
bado hakijafahamika kisha kumuua askari mmoja aliyekuwa nje ya uzio wa eneo hilo
la benki," alisema Jafary .
Hata hivyo alisema askari aliyeuawa hakuwa kazini ila
walinzi wote wa benki wapo salama na silaha zao hazikuchukuliwa.
No comments :
Post a Comment