Friday, September 4, 2015

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA USINDIKAJI WA VIUNGO VYA CHAKULA

Viungo vya chakula ni kati ya bidhaa zinazotumika kwa wingi kwa lengo la kuboresha mapishi, matibabu na kutengenezea manukato.

Kuna aina nyingi za viungo kulingana na matumizi yake. Mifano ya viungo ni pamoja na;  pilipili, iliki, mdalasini, tangawizi, manjano, jira n.k.

Viungo husifika kutokana na uwezo wake wa kutoa harufu, rangi na ladha nzuri na vimegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na sehemu ya mmea inapotokea. Kuna viungo ambavyo hutokea kwenye majani, magome, matunda, shina, mizizi, mbegu n.k

Viungo vinafaida kubwa kiafya kwa kuchangia katika kuua vijidudu waletao madhara mwilini (anti-microbial effects) na vile vile husaidia katika kutunza vyakula visiharibike.

Kwamujibu wa uchunguzi uliofanyika nchini China nakuchapishwa kwenye blog hii  matumizi ya viungo mara moja hadi mbili kwasiku inaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kufa mapema kwa asilimia 10. Taarifa hiyo unaweza kuipata HAPA.


AINA ZA VIUNGO



Kuna ina mablimbali za viungo kama vile;

• Mbegu- (jira, uwatu)
•Poda/ unga-manjano, pilipili na tangawizi
• Viungo mchanganyiko (masala)
•Uji mzito (vitunguu, tangawizi )
• Concentrates (tamarind concentrate)
• Mafuta

UFUNGASHAJI WA VIUNGO

Ili kuweza kufungasha viungo vizuri ni vyema kuzingatia aina ya matirio yatakayotumika katika ufungashaji. Aina ya materio au kifungashio inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kulinda na kuongeza ubora wa viungo.




Baadhi ya mambo yanayoweza kuchangia ubora wa viungo kuharibika ni kama vile;
 Kuvuta Unyevunyevu;

Mara nyingi viungo huwa katika hali ya ungaunga au poda. Kutokana na ukavu na hali ya ungaunga viungo vinakuwa na uwezo mkubwa wa kuvuta unyevunyevu kutoka kwenye mazingira(Hygro-scopic properties) na kusababisha viungo hivyo kutengeneza mabonge au kushikana. 

Kuvuta huku kwa unyevu kunaweza pia kuchangia katika upotevu wa ubora wa viungo hasa kupoteza hali ya ungaunga au poda.

Kupoteza harufu au ladha

Viungo vina kiwango cha mafuta ambavyo husaidia katika kuleta harufu na ladha. Kupungua kwa kiwango cha mafuta haya huchangia katika upotevu wa harufu na ladha.

Kupotea kwa kwa rangi


Viungo vingine kama iliki za kijani, pilipili nyekundu na manjano huwa na kwango fulani cha rangi. 

Mwanga husababisha upotevu mkubwa wa rangi katika viungo katika viungo hivi.

Wadudu

Wakati mwingine viungo huvamiwa na wadudu, ambapo idadi yake huweza kuongezeka iwapo viungo hivyo vitakua kuna kiwango kikubwa cha unyevunyevu, au vitahifadhiwa sehemu yenye joto na hewa ya oxygen.

Vijidudu

Iwapo viungo vitahifadhiwa kwenye sehemu yenye kiwango kikubwa cha unyevunyevu viungo huweza kuvuta unyevu. Unyevunyevu unaweza kuchangia viungo kushambuliwa na vijidudu

MAHITAJI KATIKA UFUNGASHAJI 
Ili kuweza kudhibiti ubora wa viungo vya chakula wakati wa usafirishaji, utunzaji na usambazaji ni muhimu kuma makini wakati wa uchaguzi wa vifungashio au matirio ya vifungashio.

Kazi ya vifungashi vya viungo vya chakula ni hizi zifuatazo;
• Kulinda bidhaa isishambuliwe na vijidudu au wadudu
• Kulinda bidhaa kutokana na mazingira hatarishi ya joto kali, unyevunyevu na hewa ya oksijeni.
oxygen.
•Kwa ajili ya kuboresha muonekano wa bidhaa

Kutokana na hilo vifungashio ni lazima viwe na sifa ifuatayo;

  • Uwezo mkubwa wa kuzuia unyevuyevu na hewa ya oksijeni.
  • Uwezo mkubwa wa kuzuia ladha na harufu isipotee.
  • Uwezo wa kuzuia viungo visichukue harufu na ladha kutoka kwenye mazingira.
  • Uwezo wa kuzuia upotevu wa ladha na harufu
  • Wakati mwingine viungo huwa na tabia ya kutoa mafuta ambayo hu-react na leya ya ndani ya vifungashio na wakati mwingine kusababisha kifungashio kupoteza ubora wake. Kutokana na hili ni vyema kwa vifungashi kuwa na matirio ambayo hayapitishi mafuta.
  • Vifungashio vinatakiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuruhusu uchapaji wa maandishi au lebo.
  • Uwezekano wa kufungua na lufunga mara baada ya kutumiaka.
HITIMISHO;

Viungo vya chakula/ Spices hupatikana katika aina na fomu mbalimbali. Katika jamii zetu  viungo vinafungashwa kwenye vifungashio vya karatasi, plastics n.k. 

 Suala msingi la kuzingatia ni kwamba vifungashio vinapaswa kulinda na kuhifadhi ubora wa viungo ili visipoteze rangi, harufu, ladha na muonekano wake. Kulingana na hilo vifungashio ambavyo vinapitisha mwanga (transparent) si vyema kutumika kwani vinaweza kusababisha ubora wa viungo kupotea.

No comments :

Post a Comment