Thursday, September 3, 2015

MBEGU ZA UWATU ZINASAIDIA KUREKEBISHA HEDHI KWA WANAWAKE


Mbegu za uwatu au kwa lugha ya kigeni Fenugreek, ni moja kati ya tiba-mbadala ambazo huweza kutumika katika kurekebisha hedhi za wanawake. 
Mbegu hizi zinapatikana maeneo mengi hapa duniani na Tanzania.
Mbegu hizi pia hutumika katika kutibu matatizo mbalimbali ya kiafya katika nchi mbalimbali kama vile Misri, Ugiriki, Italia na Asia ya kusini. Mbegu hizi pia hutumika kama kiungo katika mapishi .
 Mbegu za uwatu zimegundulika kuwa na virutubisho kama vile protini, vitamini, vitamin C, na madini ya potassium.

Kwakuwa mbegu hizi kuwa na tabia yakinishi za hormoni za Ostrogeni (estrogen-like properties), mbegu za uwatu zinasaidia katika kurekebisha 'moody' katika kipindi cha ukomo wa hedhi (meno-pause).

Mbegu hizi pia hutumika katika matibabu ya asthma, mfumo wa upumuaji, kurekebisha mmeng'enyo wa chakula, kuongeza nguvu za kiume, na matibabu ya ngozi.


Mbegu hizi pia hutumika katika matatizo ya uzazi, matatizo ya homoni, matibabu ya kisukari na kupunguza maumivu wakati wa hedhi




UWATU HUTUMIKA KATIKA KUPUNGUZA KIWANGO CHA CHOLESTEROL KWENYE DAMU.

Uchunguzi unaonyesha kwamba iwapo mtu atatumia gramu 56 kila siku za mbegu za uwatu itasaidia kiwango cha cholesterol kwa asilimia 14 ndani ya miezi sita na atapunguza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo kwa asilimia 25.
Mbegu hizi siyo lazima zitumiwe peke yake zinaweza kutumiwa au zikachanganywa na chakula kama vile achali n.k. vile vile zinaweza zikatumiwa kwa njia ya vidonge. 

MATIBABU YA KISUKARI NA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE DAMU.

Mbegu za uwatu zimegundulika katika kusaidia kutibu kisukari (diabetes type 2) na kusaidia katika kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu. Inashauriwa mtu atumia gramu 500 mara mbili kwa siku kila siku ili kupata matokeo mazuri.

KUTIBU MATATIZO YA NGOZI

Uchunguzi unaonyesha kwamba mbegu za uwatu husaidia katika matibabu ya matatizo ya ngozi. inashauriwa kwamba mtu atumie kijiko kimoja cha mbegu za uwatu na kusaga kuwa poda/ unga na kuchanganya na maji ya uvuguvugu na kupaka kwa kitambaa sehemu yenye jeraha au ilyoathiriwa.

MATIBABU YA KIUNGULIA

Mbegu za uwatu zinakiwango kikubwa cha uteute ambao husaidi katika kupunguza kiungulia kutokana na kuzuia asidi iliyopo tumboni isikutane na kuta za tumbo na utumbo.
Inashauriwa mtu kuchanganya kijiko kimoja cha chai simply  cha mbege za uwatu kwenye chakula. Njia nyingine ni kunywa kijiko kimoja cha chai cha mbegu hizi na  sprinkle 1 na maji au juisi.

MATIBABU YA HOMA

Mbegu za uwatu hutumika katika kupunguza homa iwapo zitatumika pamoja na maji ya limao au asali.
Ili kutibu homa inatakiwa mtu kutumia kijiko kimoja cha uwatu mara tatu kwa siku pamoja na chai (green tea), pamoja na kijiko kimoja cha asali na juisi ya limao.
KUONGEZA UKUBWA WA MAZIWA/MATITI

Mbegu za uwatu hutumiwa pamoja na bidhaa zingine katika kusaidia kurekebisha kiwango cha homoni katika mwili na hivyo kuongeza ukubwa wa maziwa au matiti. Ili kupata matokeo mazuri inatakiwa kufanya mbegu za uwatu kuwa sehemu ya mlo wako. Inashauriwa mtu atumie gramu 3 za uwatu kwa siku

No comments :

Post a Comment