Friday, June 26, 2015

SIDO YANDAA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA USINDIKAJI WA VYAKULA

Shirika la Kuudumia Viwanda Vidogo (SIDO) limeandaa mafunzo ya ujasiriamali na usindikaji wa vyakula yatakayofanyika mwezi wa nane mwanzoni katika ofisi zake zilizopo Vingunguti Dar es salaam.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zinazohusiana na ujasiriamali na usindikaji wa vyakula zitafundishwa na wataalamu mbalimbali wa shirika hilo kama vile Wataalamu wa Vyakula na wataalamu wa Biashara. Kati ya mada zitakazofundishwa ni mbinu za kibiashara na mahitaji ya kisheria ili kuwezesha ufanyaji wa baiashara wenye tija na wenye kufuata sharia.
Njia pekee ya kukuwezesha kuhudhuria mafunzo hayo ni kufika Ofisi za SIDO zilizopo vingunguti na Upanga ili kupata maelezo zaidi na kujiandikisha.

No comments :

Post a Comment