MBUNGE wa viti maalum ( CCM ), mkoa wa Dodoma Mariam Mfaki amefariki dunia leo katika hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kifo hicho mjini hapa mtoto wa marehemu, Mohamed Mfaki amesema kuwa mama yake alilazwa juzi usiku hospitalini hapo akisumbuliwa na tatizo la kansa ya utumbo na mapafu.
Marehemu Mfaki amekuwa mbunge wa viti maalum kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.
“Awali kabla marehemu mama hajawa mbunge alikuwa Katibu tarafa kwa muda wa miaka 20 ambapo alistaafu mwaka 1987 na baadae aliingia kwenye siasa,” amesema Mohamed.
Marehemu Mfaki alizaliwa mwaka 1947 ameacha mume, watoto sita na wajukuu 10.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu amesema kuwa taratibu za mazishi zinafanyika leo (kesho) saa kumi ambapo atazikwa shambani kwake Miyuji.
Aidha, Mohamed amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu Area E karibu na Summit hotel mjini hapa.
No comments :
Post a Comment