Wednesday, July 22, 2015

AMISOM YAUKOMBOA MJI WA GEDO SOMALIA

Mji wa Baardheere ulioko eneo la Gedo nchini Somalia umekombolewa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika AMISOM, ikiwa ni mara ya kwanza kwa miaka saba.
Wapiganaji wa Al Shabaab wamekua wakiuthibiti mji huo tangu mwaka wa
2008. Wanajeshi wa Kenya wakisaidiwa na helikopta za kivita wameonekana wakiingia mjini humo.
Wakaazi wengi wamekimbilia vijiji vya mbali. Wakati huohuo Kiongozi wa kiasili kutoka Somalia Kusini amesema kuwa makumi ya watu wamefariki katika eneo hilo kufuatia mapigano makali.
Hivi majuzi Wanajeshi wa Muungano wa Afrika, Amisom, wakishirkiana na wanajeshi wa Somalia walianzisha mashambulizi makali katika maeneo yanayokaliwa na makundi ya Al Shaabab.
Somalia                     
Makabiliano ya siku tatu zilizopita yamekuwa yakilenga maeneo ya Gedo na Bokool.
Mwanajeshi mmoja wa Somalia, Kanali Abdirahim, Mohammed Osman, amesema kuwa wanachama 30 wa Al Shaabab na afisa mmoja wa jeshi wameuawa katika makabiliano hayo.
Hakuna aliyethibitisha habari hizo, lakini kuna ushahidi kuwa watu wengi wametimuliwa makwao kutokana na makabiliano hayo.

No comments :

Post a Comment