Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Israel Natse, amejitoa rasmi katika siasa na kurudia kazi yake ya uchungaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini.
“Mimi ninarudi kwenye kazi yangu ya uchungaji naachana na siasa, huu ndiyo wito wangu nilioitiwa na mungu wa uchungaji,” alisema.
Akizungumza kwa njia ya simu ya kiganjani, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro, alisema kwa Jimbo la Karatu waliochukua fomu za kugombea ubunge ni Lazaro Masai, Fransisca Duwe, William Kumbalo, Kwamala Aloyce na Pascal Gutt.
No comments :
Post a Comment