Sunday, July 19, 2015

DUKA LA WESTGATE LAFUNGULIWA

Nairobi: Duka la Westagate lililo mji mkuu wa Kenya Nairobi hatimaye limefunguliwa miaka miwili tangu lishambuliwe na wanamgambo wa Al shabaab.
Watu 67 waliuawa wakati wa makabiliano ya siku nne wakati wanamgambo hao walipowafyatulia risasi wateja.
Duka hilo linafunguliwa wiki moja kabla ya rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara nchini Kenya hatua inayoonekana kama ishara ya imani kwa usalama wa nchini Kenya.
Al Shabaab wameendesha mashambulizi mengine mabaya nchini Kenya tangu litokee shambulizi la Westgate likiwemo la chuo kikuu cha Garissa ambapo watu 150 waliuawa.

No comments :

Post a Comment