Monday, July 6, 2015

UKWELI KUHUSU MATUMIZI YA KAHAWA.

http://emanuelcosmas.blogspot.com/
Na. Emanuel

Utangulizi

 
Kahawa ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi duniani.  Kwa mujibu wa jarida la Worldatlas takwimu za mwaka 2013 kati ya nchi kumi zenye matumizi makubwa ya kahawa,  nchi inayoongoza zaidi kwa matumizi ya kahawa ni Finland ambayo ina wastani wa vikombe 2.64 vya kahawa vinavyonywewa  kwa siku (kilo 9.6 kwa mwaka) kwa kila raia. Nchi zingine tano zinazoongoza kwa matumizi ya kahawa ni Norway namba 2 (Kilo 7.2 kwa mwaka)), Netherland  namba 3 (Kilo 6.7 kwa mwaka), Slovenia 4 (kilo 6.1 kwa mwaka) , na Austria namba 5 (kilo 5.5 kwa mwaka) kwa kila raia.
 
Kuna mambo mengi huwa yanazungumzwa kuhusu kahawa. Mengine ni ya kweli na mengine si ya kweli. Leo hii nitaongelea vyote hivyo ili kuweka uwazi kuhusu kahawa.

1. KUNA HABARI KWAMBA MTU ANAWEZA KUWA ADDICTED NA KAHAWA.

Hakuna ukweli kuhusu hili. Kahawa/ Caffein humfanya mtu achangamke kwa huchangamsha mfumo wa fahamu au kwa kitaalamu Central nervous System. Utumiaji wake wa mara kwa mara humfanya mtu apende kutumia zaidi, hata hivyo Utumiaji wa kahawa hauwezi mfanya mtu apate shida yeyote  kama vile ambavyo inawapata watumiaji wa madawa ya kulevya .

Kama mtumiaji wa kahawa ataacha kunywa kwa ghafla anaweza akapata shida kidogo au dalili fulani  kwa siku moja au zaidi iwapo alizoea kunywa vikombe viwili au zaidi kwa siku moja. Dalili zingine ni
  • Kuumwa kichwa     
  • Uchovu au kuchoka     
  • Kukosa mudy
  • Kuwa mwenye mawazo     
  • Na ugumu katika ku-concentrate

2. KAHAWA HUKOSESHA USINGIZI (INSOMNIA)

Mtu anapokunywa kahawa, caffein huingia kwa haraka katika mfumo wa damu. Vilevile mwili huitoa caffeine kwa haraka kupitia maini.
Kwa kawaida mwili huchukua masaaa matano hadi saa saba kuondoa nusu ya kiwango cha caffeine iliyoingia kwenye mwili. Baada ya masaa nane  hadi kumi, 75% ya caffeine inakua imeshaondolewa kwenye mwili. Kwa watu wengi kikombe kimoja cha kahawa alichokunywa asubuhi hakiwezi mzuia kupata usingizi usiku.

Unywaji wa kahawa mida ya usiku inaweza ikamsababishia mtu kutokupata usingizi kwa muda muafaka. Kwa waliowengi unywaji wa kahawa masaa sita kabla ya muda wa kulala haiwezi msababishia matatizo katika kupata usingizi, ingawa hii itategemeana na wingi wa kahawa iliyotumiwa na uwezo wa mwili kuichakata hiyo kahawa
   

3. KAHAWA INAWEZA KUMSABABISHIA MTU MATATIZO YA MOYO, MIFUPA KUWA MEPESI (MILALINI) NA KANSA

Unywaji wa kahawa kwa kiwango kidogo kikombe kimoja hadi vitatu haiwezi msababishia matatizo kiafya. Ingawa kuna watu ambao wanakua ni rahisi kupata matatizo ya kiafya kama vile watu wenye pressure ya damu au wazee.
 
Kulainika kwa mifupa kunaweza kutokea iwapo kiwango kikubwa cha kahawa kitatumiwa kama vile 744 milligram kwa siku. Kahawa huongeza upotevu wa kiwango kikubwa  cha madini ya calcium na magnesium kupitia mkojo. Tafiti zinaonyesha kamba upotevu huu hauwezi kumletea shida mtu iwapo anapata mbadala ambao utarudisha madini hayo mwilini kama vile matumizi ya maziwa au kuchanganya kahawa na maziwa.

Watu wazima wanahatari zaidi ya kupata madhara iwapo watatumia kahawa. Watu wazima wanaweza pata matatizo kama vile ya kuvunjika kwa mifupa ya nyonga ingawa watafiti bado hawajapata uhusiano kati ya matumizi ya kahawa na kuvunjika kwa mifupa ya nyonga. Iwapo una umri mkubwa ni vyema ukapata ushauri wa madaktari au wataalamu wa afya.
 
Matumizi ya kahawa vilevile husababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo na presha ya damu kwa watu ambao wapo sensitive sana na kahawa. Ingawa tafiti nyingi hazionyeshi uhusiano wa moja kwa moja baina ya kahawa na kuongezekea kwa cholesterol, kubadilika kwa mapigo ya moyo au kuongezeka kwa matatizo katika mzunguko wa damu.

Kama wewe tayari unamatatizo ya presha ya damu au matatizo ya moyo, ni vyema ukapata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari au wataalamu wengine wa afya kuhusiana na matumizi ya kahawa.
 
Tafiti 13 zilizowahusisha watu 20,000 hazionyeshi uhusiano kati ya kansa na cafffein. Kwa upande mwingine kahawa inaweza ikasadia kuzuia aina fulani fulani za kansa

4. KAHAWA NI HATARI KWA WANAWAKE WANAOTAKA KUBEBA MIMBA

Tafiti nyingi hazionyeshi uhusiano kati ya na matumizi ya kahawa na haya yafuatayo;

  • Kushindwa kuzaa
  • Kutoka kwa mimba       
  • Kuzaa mtoto mwenye matatizo       
  • Kuzaa kabla ya wakati
  • Kupungua kwa uwezo wa kuzaa
Kw wajawazito au wanaotaka kupata ujauzito haushauriwa kutumia zaidi ya milligram 200 kwa siku (siyo zaidi ya vikombe viwili vya chai). Hii ni kwa sababu mwanamke akizidisha kiwango cha kahawa kunauwezekano mkubwa kwa mimba kutoka. 

5. KAHAWA HUSABABISHA MTU KUPUNGUKIWA NA MAJI

Unywaji wa kahawa unaweza mfanya mtu akapata haja ndogo kwa kiasi kikubwa, ingawa kiwango cha maji utakachopoteza kinaweza kufidiwa na kiwango cha maji utakachopata kwa hicho kinywaji.

6. KAHAWA HAIFAI FAIDA KWA AFYA

Kuna faida chache za kahawa ambazo zimethibitishwa kitaalamu. Wengi wa watumiaji wa kahawa wanatoa ushuhuda ya kwamba kahawa inaongezea uchangamfu, concentration, na nguvu. Moja ya watafiti kutoka Ufaransa wametoa majibu kwamba wengi wa wanawake watumiaji wakubwa wa kahawa wamekua wanapoteza uwezo wa utambuzi (cognition abilities). Kwa upande mwingine kahawa imeonekana kusaidia katika kupunguza maumivu ya kichwa.
Kuna ushaidi mwingine unaonyesha kwamba, kahawa inaweza kusaidia haya yafuatayo;     

  • Magonjwa ya maini
  • Kisukari     

Hitimisho

Ingawa kahawa inafaida nyingi kiafya ni vyema kukumbuka kahawa inaweza kukuletea madhara kiafya. Hivyo wakati bado tafiti zinafanyika ni vyema kuhakikisha matumizi ya kahawa hayazidi kiwango na kufuata ushauri wa wataalamu katika matumizi ake ili kujiepushia madhara ambayo yanaweza kutupata.

No comments :

Post a Comment