Sunday, July 19, 2015

JANUARI MAKAMBA AMTUNISHIA MISULI KINGUNGE

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amemtolea uvivu mshauri wa zamani wa Siasa wa Rais Jakaya Kikwete, Kingunge Ngombale-Mwiru kwa kuupinga mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM na kusema anakivuruga chama.
Kingunge aliyejitoa kindakindaki kumpigania mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa, amekuwa akitoa matamko mbalimbali kuhusiana na mchakato huo na zaidi akisema haukutenda haki hasa baada ya kuenguliwa jina la Lowassa.
Kamati ya Usalama na Maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, ndizo zilizokuwa na kazi ya kuchuja majina hadi kupatikana mgombea mmoja, Dk John Magufuli.
Akizungumza jana kwa simu kutoka Bumbuli Tanga, Makamba (pichani) alisema: “Mzee Kingunge ni mtu mzima, ninamuheshimu sana, ni mkongwe katika siasa, lakini anakivuruga chama.”
Alisema binafsi hakubaliani na kauli za Kingunge kupinga uteuzi wa Dk Magufuli kwa sababu makada wote wa chama waliokuwapo Dodoma, waliamua kumpitisha kwa kuwa walimuona anafaa na anaweza kukijenga chama.
“Ndani ya chama kuna wazee wenye busara ambao waliangalia vitu vingi hadi kumteua mgombea kwani unaweza kuwa mtendaji mzuri lakini ukawa na kasoro nyingi hivyo, unaweza vilevile kuonekana ukashindwa kukivusha chama kwenye ushindi"
“Mimi ninamuheshimu sana Mzee Kingunge, lakini siwezi kukubaliana naye anavyokandia mchakato. Mimi ninaamini ulikuwa sahihi, kila mtu ameridhika na ndiyo maana kura zilipigwa…, tuna imani naye na anaweza kuongoza tangu zamani,” alisema Makamba.
 Makamba alisema, ana imani kwamba atafanya vizuri hivyo ni bora apewe ushirikiano kama walivyopewa viongozi waliopita ili kukinusuru Chama cha Mapinduzi na watu waendelee kukiheshimu kama awali.
 Katibu mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba alikaririwa na vyombo vya habari juzi akisema kwamba, watu wanaoendelea kulalamikia mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Magufuli wana masilahi binafsi na siyo kwa ajili ya kukiimarisha chama hicho.
Kauli ya Kingunge
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake mwanzoni mwa wiki, Katibu huyo wa zamani wa halmashauri kuu ya CCM alisema, Kamati ya Usalama na Maadili iliteka majukumu ya Kamati Kuu baada ya kuamua kuchuja majina ya makada waliojitokeza kuwania urais hadi kufikia watano, akisema jitihada hizo zilifanywa kwa kuvunja kanuni na zililenga kumuengua Lowassa kuwania kuingia Ikulu.
 Kingunge alisema kitendo cha kumuengua Lowassa kwa kuvunja kanuni kimeacha kasoro kubwa ndani ya chama hicho tawala kwa sababu taratibu zilikiukwa ili kupata viongozi.
 Alisema kosa hilo siyo la Dk Magufuli aliyepitishwa kuwa mgombea urais wa CCM, na wala si la Lowassa, bali ni la waliopendekeza majina ya walioingia tano bora.
 Jina la Lowassa, ambaye alijidhihirisha kukubalika ndani na nje ya CCM kutokana na harakati zake za kusaka wadhamini kujaa watu, halikupelekwa kwenye Kamati Kuu, kwa mujibu wa Kingunge na hivyo kutojadiliwa na chombo hicho ambacho kilimpitisha Dk Magufuli, Dk Asha-Rose Migiro, January Makamba, Bernard Membe na Balozi Amina Salum Ali

No comments :

Post a Comment