Monday, July 27, 2015

BURUNDI: AGATHON RWASA AHUDHURIA BUNGE

AGATHON RWASA
Kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa amehudhuria kikao cha kwanza cha bunge tangu uchaguzi wa ubunge mnamo tarehe 29 juni.
Hatua hiyo imewashangaza wengi kwa kuwa alipinga matokeo ya uchaguzi huo pamoja na yale ya urais wiki iliopita ambapo alijipatia asilimia 20 ya kura.
Lakini viti 12 kati ya 30 vya muungano wake havikuwa na wabunge huku wabunge walio watiifu kwa kiongozi mwenza Charles Nditije wakisusia kikao hicho.

No comments :

Post a Comment