Monday, July 27, 2015

KAMA NI KWELI LOWASSA SIYO FISADI,JE NI KIPI KITATOKEA IWAPO LOWASSA ATAKUWA RAISI ?


 
Kwa nini Lowasa alipokuwa CCM aliitwa fisadi, hii ni kwa sababu yeye kama waziri mkuu, msimamizi mkuu wa serikali alitakiwa akemee inshu zote za Ufisadi ikiwemo ile ishu
ya RICHMOND. Kuna ambao wanasema kwamba lowassa alipata shinikizo kutoka sehemu fulani ili kuokoa mambo yasiharibike.

 Je! iwapo Lowassa atafanikiwa kuwa raisi kupitia UKAWA ataweza kuongea ukweli wa kilichotokea?
Kuna mambo mengi sana yametokea ndani ya nchi ambayo mengi yao bado ni kizungumkuti baina ya watanzania. 

Je! tupate imani kwamba Iwapo Lowassa atakuwa raisi tutajua ukweli kuhusu Richmond?

Je! Ataongea Vitu vyote ambavyo Mwakyembe aliviacha Kuongea katika Riport yake ,Kwa kuilinda Ikulu. Je, ataweza kuongea kuhusu wamiliki Halisi wa IPTL?

Vipi kuhusu Mambo ya Escrow ? 

Je! tutajua ni nani aliye-engineer Mchakato wote wa Escrow?

Je! Ataelezea ni nani Anamiliki Kampuni ya Simba Trust, iliyochukua Bilion 75 kwenye Kashifa ya Escrow. 

Riport yote ya Takukuru ipo hewani kuhusu Esrow.

 Lowassa  anatubu na anarudi CHADEMA ambao wanadai wanataka kuitetea nchi.  Kama Lowassa siyo fisadi je atatuambia fisadii mkuu wa hii nchi ni nani? 

Mimi na wewe tukae mkao wa kula, cha msingi;

 KURA YAKO NDIYO ITAKAYO AMUA MUSTAKABALI WA NCHI YETU INAPOELEKEA!!!

No comments :

Post a Comment