Wednesday, July 8, 2015

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari apata ajali


Arumeru: Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amepata ajali ya helikopta aliyokuwa akiitumia kufanya ziara jimboni kwake hii leo.

Habari kutoka Arumeru zinasema kuwa helikopta hiyo ilipoteza mwelekeo na kwenda kugonga mti na kunasa juu ya mti huo.

Aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo na rubani wake
 
walitoka wakiwa wazima na wapo katika Hospitali ya Kanisa la Kilutheri ya Selian ya jijini Arusha. Abiria wawili, mmoja anajulikana kwa jina la Eve ambaye ni mmoja wa viongozi wa BAWACHA jimboni, ameumia mbavu na mwingine kuvunjika mguu.
  

Source:

No comments :

Post a Comment