DODOMA: Mtu mmoja mwenye asili ya Kihindi alikamatwa jana akiwa na mabilioni ya pesa Mjini Dodoma. Mitandao mingi ya kijamii iliripoti kwamba 'Mdosi 'huyo pia kingine alikamatwa na simu ikiwa na maelekezo kwamba pesa hizo ni za kuwapatia Wajumbe.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya uhakika au iliyotolewa
rasmi na vyombo vya usalama, kuhusu ni nani aliyekamatwa na makusudio ya kubeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na uhusiano wake na vikao vya CCM vinavyoendelea huko Dodoma.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya uhakika au iliyotolewa
rasmi na vyombo vya usalama, kuhusu ni nani aliyekamatwa na makusudio ya kubeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na uhusiano wake na vikao vya CCM vinavyoendelea huko Dodoma.
Hadi hivi sasa taarifa bado zinakinzana kuhusu ni nani hasa anahusika kwenye fedha hizo ndefu ambapo katia pitapita zangu za kwenye mitandao ya kijamii niliweza kuzinyaka habari hizi mbili ambazo zinakinzana;
Blogu ya KajunaSon inasema:
"Katika hali ya kushangaza mtu mmoja mwenye asili ya Kuburushi ambaye jina lake halikuweza kupatikana leo amekamatwa na marundo ya hela kwenye begi ikiwa amefika nazo kwa ajili ya kuzigawa kwa wajumbe wa NEC ili wasusie kikao cha leo hadi pale jina la Mhe. Edward Lowassa litakaporudishwa na kama ikishindikana achaguliwe Mhe. Magufuli."Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na makachero wenu waliopo maeneo mbali mbali ya mji wa Dodoma zinasema kuwa watu hao walikamatwa katika hoteli ya St. Gasper iliyopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Mpaka sasa hali si shwari kwa mji wa Dodoma maana vijana wengi wamezagaa kila kona huku ulinzi ukiwa umeimalishwa.Mhindi huyo alishukia kwenye hoteli ya St. Gasper ambayo wapambe wengi wa Lowassa wakiwamo mzee Kingunge ambaye wamepiga kambi.Huyo Mburushi ni mtumishi wa Caspian ya Rostam Aziz. Wengine walioonekana pichani wamo Fadhili Ngajiro; Ole Porokwa; Omar Ng'wanang'wala.
Blogu ya Malunde1 inasema:
Video hapa chini inaonyesha majibu ya mdosi huyo, alipoulizwa ametokea wapi na nani amemtuma."Kuhusu taarifa za kijana aliyenaswa na masanduku ya fedha upekuzi bado unaendelea kwenye eneo la tukio ambo taarifa zisiso rasmi zinadai kuwa kijana huyo alikamatwa na wafuasi wa Mh.LOWASSA ambao waliweza kuripoti Polisi na Takukuru na inadaiwa kuwa fedha hizo zilipelekwa kwa ajili ya kugawia wajumbe waweze kumchagua mmoja wa wagombea.Aliyekamatwa kageuka, anasema katumwa na MembeTaarifa zaidi tutawafahamisha kadiri zitakavyo thibitishwa na mamlaka zinazoendelea na Uchunguzi."
Picha zingine za tukio lililovuta hisia za wengi zipo hapo chini
No comments :
Post a Comment