Dodoma: HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kazi yake ya kuteua majina matatu ya wagombea wa CCM, ambayo hayakutarajiwa na wengi. NEC imewatupa nje, wagombea Bernard Membe na Januari Makamba.
Magufuli ndiye aliyeibuka kinara baada ya kupata kura 290, wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Balozi Amina aliyepata kura 284, nafasi ya tatu ilishikwa na Dk. Migiro aliyepata kura 280, wakati nafasi ya nne ilienda kwa Makamba aliyepata kura 124 na Membe aliambulia kura 120.
Wagombea hao watatu watachuana kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho kwa kupigiwa kura ili kumpata mmoja ambaye atapeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 uliopangwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Kikao hicho ambacho kilianza kwa hofu kutokana na wanaosadikika kuwa ni wapambe wa Edward Lowassa kuimba wimbo wa uliomtukuza mgombea wao kwa kusema “tuna imani na Lowassa” haukusimama hata alipokuwa anaingia ukumbini Mwenyekiti Kikwete, ambapo alishuhudia kisicho cha kawaida kikiendelea.
Pamoja na sintofahamu hiyo lakini wazee wastaafu walioingia ukumbini walikubaliana na tafrani hiyo ni marais na wenyeviti wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, makamu wenyeviti Amani Karume, John Malecela, Cleopa Msuya, Pius Msekwa na waziri mkuu mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim.
Busara za wazee hao ndiyo zilizofanya kikao hicho kumalizika kwa amani na kuwapata wagombea watatu ambao wataenda kumtoa mgombea mmoja.
No comments :
Post a Comment