Sunday, July 12, 2015

MGOMBEA GANI WA CCM ATAKAYEWEZA KUPAMBANA NA KISIKI CHA DR. SLAA

Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya Halmashauri kuu ya CCM haijamtangazea mteuliwa atakayegombea nafasi ya uraisi kupitia tiketi ya CCM, hali bado ni tete katika vichwa vya watu,  wengi wao wakitafakari na kujiuliza ninani hasa atakayeteuliwa ili kuchuana na Dr. Slaa. 

Hii inatokana na matokeo ya uteuzi yasiyotabirika, na kutokana na ukweli kwamba mtu yeyote kati ya watatu waliobaki anaweza kuteuliwa kuiwakilisha CCM. Baada ya tano bora kutangazwa watu wengi walitabiri kwamba Membe ndiye angeshika usukani lakini kutokana na Membe kutolewa kwenye kinyang'anyiro bado hali ya sintofahamu imendelea kutalawa vichwa vya watu hasa wenye chama chao.

Katika uchaguzi wa mwaka huu kumetabiriwa kuwapo kwa upinzani mkubwa mkubwa baina ya CCM na UKAWA ambapo kwa upande wa UKAWA Dr. Slaa ndiye atakaye shika kijiti. Kutokana na umashuhuri wa kisiasa wa Dr. Slaa bado swali hili ni gumu kulijibu la kwamba ni nani hasa atakayeweza kukiruka kisiki cha mgombea huyo.

Watu watatu waliobaki wanaowania nafasi moja ya kukiwakilisha chama cha CCM ni pamoja na Dr. Magufuli, Asha Rose Migiro na Amina S. Ali. Ambapo Dr. Magufuli anapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Dr. Slaa ni kati ya wagombea ambao walikua tishio katika chaguzi zilizopita hasa hasa ile ya mwaka 2010 ambapo alichuana vikali na Jakaya Kikwete.

Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

Dakika chache zilipita na Dr. Slaa akaamua kuthibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa twitter na kuandika 

Nashukuru UKAWA kwa imani kubwa. Kazi ya mabadiliko iliyoanza 1992 kwa vyama vingi imebakiza miezi michache kushinda. Kura yako ni ukombozi –  @willibrordslaa

Matokeo ya mteule wa CCM yanatarajiwa kutolewa leo saa nne

No comments :

Post a Comment