Tuesday, August 4, 2015

UN:Shambulio la Burundi lichunguzwe



Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametaka uchunguzi wa kina ufanywe kwa
shambulio lililofanywa dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi.

Pierre Claver Mbonimpa(Kwenye Picha) alijeruhiwa vibaya baada ya mtu aliyejihami kumpiga risasi usoni na kutoroka kwa pikipiki.

Mwanawe Mbonimpa, Amandine Nasagarare ameambia BBC kuwa babake bado amelazwa hospitalini japo hali yake sasa imeimarishwa.

No comments :

Post a Comment