Katika hali ya kustaajabisha Sungura aliweza kupambana na nyoka mkubwa aliyekua amemkamata mtoto wake tayari kwa kumfanya KITOWEO. Nyoka huyo mwenye njaa na mwenye meno namagamba mekundu alikua amembananisha sungura huyo mtoto kistadi na kumfanya asiweze kufurukuta.
Katika Video hiyo ya kustaajabisha ilipostiwa kwenye You Tube ilimuonyesha mama sungura akiwa mwenye ushupavu na hasira akimvaa nyoka huyo aliyekua tayari amemuweka kwenye himaya sungura mtoto.
Nyoka huyo aliona siyo tabu na kuamua kumuachia mtoto na kusepa mara baada ya kuona "PUNCH" za mama sungura zimemzidia. Video haionyeshi ni aina gani ya nyoka aliyehusika kwenye tukio hilo.
Angalia video hapo chini uone kilichojiri.
T:
No comments :
Post a Comment