Dar/Mikoani. Siku chache baada ya kutangaza kuridhika na mapendekezo ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kutompitisha kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyang’anyiro cha urais, Charles Makongoro Nyerere amejitosa
kuwania ubunge katika Jimbo la Kawe, Dar es Salaam.
Pia, Profesa Sospeter Muhongo ambaye naye alikuwa miongoni mwa wagombea urais wa CCM, alichukua fomu ya kuwania Ubunge wa Musoma Vijijini. Baada ya kuchukua fomu, Waziri huyo wa zamani wa Nishati na Madini aliandika katika ukurasa wake wa Facebook: “Leo nimechukua fomu nagombea ubunge wa Musoma Vijijini bado ninadhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania. Tusikate tamaa.”
Aidha, aliyekuwa mgombea urais mwingine, Peter Nyalali amechukua fomu kuwania ubunge Jimbo la Mbagala, sanjari na Mwichumu Msomi na Dominic Francis Haule.
Baadhi ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Katibu wa Rais ni miongoni mwa waliojitokeza jana kuwania ubunge maeneo mbalimbali nchini.
Kawe: Mbali ya Makongoro, makada wengine 14 walijitokeza kuwania kiti hicho wakiwemo; Mtiti Butiku, Yusuph Nassoro, John Mayanja, Dickson Muze na Dk Wilson Babyebonela.
Kinondoni: Emmanuel Makene.
Ubungo: Hawa Ng’umbi na Jackson Mllengo.
Kibamba: Issa Mtemvu, Felix Mdessa, Didas Lunyungu na Stanslaus Maganga.
Ilala: Mrisho Gambo
Segerea: Nicholaus Haule na Baraka Omary.
Ukonga: Amina Mkono, Edwin Moses na Robert Masegese.
Dodoma Mjini: Haidari Gulamali.
Mbeya Mjini, Mbunge wa sasa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Christopher Nyenyembe, Lazaro Mwankemwa, Charles Mwakipesile, Mchungaji Jackson Numbi, Ulimboka Mwakilili, Stephen Mwakwenda, Aman Kajuna na Aggrey Mwasanguti.
Mbeya Vijijini: Anderson Kabenga, Boniface Mwalwego na aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Lackson Mwanjale.
Moses Mwaigaga, Chance Mwaikambo, Franco Mwalutende, William Msokwa, Stephano Mwandiga, Frank Mwaisumbe, Elias Kwimba, Anthony Mwaselela, Wila Jocob, John Mwamengo, Jeremiah Mwaweza, Hardson Sheyo, Emmanuel Shonyela, Alimu Mwasile, Adam Zella, Nhungo Jisandu, Daud Mponzi na Cyprian Magulu.
Kyela: Leonard Mwaikambo, John Mwaipopo na Gwakisa Mwandembwa
Mbarali: Mbunge wa jimbo hilo, Modestus Kilufi, Michael Kalenge, Haroun Mula, Injinia Burton Kihaka na Geofrey Mwangulumbi.
Moshi Vijijini: Anthony Komu, Godlisten Malisa, Joseph Nubi, Deogratius Mushi, Clemence Chuwa, Lucy Owenya, Nicholaus Ngowi, Evarist Kiwia na Ernest Kyambo.
Vunjo: Exaud Makyao.
Mwanga: ni Henry Kileo, Joyce Mfinanga, Mengi Kigombe, Adiel Adiel na Dk Ngoma Karua.
Same Mashariki: Onesmo Fue, Mchungaji Charles Kanyika, Allan Mmamji na Naghenjwa Kaboyoka.
Same Magharibi: Christopher Mbajo, Mhina Joel, Elisafi Godson, Erick Kazoka, Gervas Mgonja na Jonas Kadeghe.
Siha: Dk Godwin Mollel, Humphrey Tuni, Aminiel Iliso na Elvis Mosi.
Kalenga: Mbunge wa sasa, Godfrey Mgimwa, Jackson Kiswaga, Abbas Kandoro, Grace Tendega, Sinkala Lucas, Mussa Mdede na Mwanahamisi Muyinga.
No comments :
Post a Comment