Wednesday, July 1, 2015

BIDHAA ZA TRICE INVESTMENTMENT CO. LTD ZAWA KIVUTIO KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

 Na Mwandishi wetu;
 Bidhaa mchanganyiko za TRICE INVESTMENT LTD zimekua kivutio kikubwa katika maonyesho ya mwaka huu ya 39 ya sabasaba. Kampuni hii iliyoanzishwa mwanzoni mwa mwaka 2010,  iliweza kuingia kwa kasi na kuthibitisha ushindani wake katika soko. Kwa mwaka huu kampuni hii inaonyesha bidhaa zake katika Jengo la Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).
 

Akiongea na ONE CLICK Habari, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni Edatrice Sinkala, amesema kwamba watu wengi wamevutiwa katika banda lake kutokana na ubora wa bidhaa zake. Nikimnukuu mkurugenzi mkuu amesema "bidhaa zangu zinatengenezwa kwa kutumia malighafi halisi nawashauri watanzania kuendelee kutumia bidhaa zangu na kuachana na bidhaa za mitaani zilizojaa uchakachuaji"

Baadhi ya bidhaa anazozionyesha ni bidhaa za chakula kama vile Tomato Sauce, Chill Sauce, Tomato paste na Peanut Butter. Ameongeza na kusema kwamba bado anawakaribisha wateja na watazamaji kwa wingi ili waweze kujionea ubunifu na bidhaa zenye ubora za kizalendo.
Baadhi ya bidhaa za Trice Investment Ltd zinaonekana kwenye picha hapo chini. 
  

Mkurugenzi Mkuu wa Trice Investment  Co. Ltd akiwa kwenye Ubora wake.

 

 

No comments :

Post a Comment