Katibu mkuu wa Shirikisho la soka la Africa Mashariki na Kati CECAFA Bwana Nicholas Musonye amekanusha uvumi kwamba CECAFA imeamua kumpigia kampeni
Magufuli kutokana na kumwalika kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya CECAFA inayotarajia kuanza kesho tarehe 18/ 07 mpaka tarehe 2/ 08.
Magufuli kutokana na kumwalika kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya CECAFA inayotarajia kuanza kesho tarehe 18/ 07 mpaka tarehe 2/ 08.
Akizungumza na waandishi wa habari Bwana Nicholas amesema kwamba wameamua kumualika Dr. Magufuli siyo kwa sababu wanataka kumpigia kampeni bali ni kutokana na nafasi yake kama watanzania wengine kwani sera ya CECAFA hairuhusu kumpigia mtu yeyote kampeniza kisiasa.
Vilabu vipatavyo 13 vinatarajiwa kushiriki katika michuano hiyo ya wiki mbili ambayo itaonyeshwa kupitia Superspot. Mshindiwa michuano hiyo anatarajia kunyakua kitita cha dola za kimarekani zipatazo elfu 60.
No comments :
Post a Comment