Thursday, July 2, 2015

JUISI YA MIWA INAWEZA KUSAIDIA KUBORESHA AFYA YAKO

Na. Emanuel Cosmas
                                                                         

Utangulizi

Unapopita maeneo mengi ya mijini na pembezoni wa miji utakutana na wafanya biashara wa miwa wanaouza miwa na wanaouza juice ya miwa. Wengi hununua juisi ya miwa kwa kuwa hufuraia utamu wake. Lakini umeshajiuliza juisi ya miwa inafaida gani kiafya?

Faida za kiafya za juisi ya miwa

Kunafaida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo;



1. Uwezo wa kuipa miili nguvu kwa haraka "instant kick of energy"

Juisi ya miwa inauwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwahiyo wakati mwingine ukiwa na nguvu au uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa. 
  

2. Juisi ya miwa ni nzuri kwa watu wenye Kisukari


Ingawa jusi ya miwa ina utamu inafaa sana kwa watu wenye kisukari. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa "Low Glycemic Index". Kutokana na hilo jusi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani. Ni mhimu pia kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa daktari.

    3. Juisi ya miwa inasaidia kupunguza matatizo ya kansa

 Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma n manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume "Prostate cancer" na kansa ya maziwa "Breast Canser"

 4. Juisi ya miwa huipatia miili  protein

Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.
Juisi a miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono "STDs" na kidney stones.

5. Juisi ya miwa inasaidia kupambana na maambukizi na kuimarisha kinga ya mwili.

Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana Ma-daktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano,
     

6. Juisi ya miwa husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula.

Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa ch madini ya potassium ambayo husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula. Vilevile juisi ya miwa husaidia kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo. Vilevile husaidia katika kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa "constipation".   

7. Juisi ya miwa husaidia kuzuia kuoza kwa meno

Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meo kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na  kuwa na kiasi kikubwa cha madini. Kwa hyo kama unafikiria kwenda kwa daltari kung'arisha meno yako, kunywa juisi ya miwa mara kwa mara.

 8. Juisi ya miwa husaidia kuimarisha ngozi.

Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung'arisha ngozi. Juisi ya miwa huweza kutumika kama " face mask na scrub" kwa kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing'arisha na kuiimarisha.

Hitimisho

juisi ya miwa inafaida nyingi mwilini, ni muhimu kuhakikisha usafi katika utengenezaji wake. Juisi ya miwa isiyokuwa salama inaweza ikawa ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya tumbo na kuhara.
.

No comments :

Post a Comment