Thursday, July 30, 2015

KWANINI DR. SLAA, TUNDU LISU NA MNYIKA HAWAKUWEPO WAKATI WA KUMKARIBISHA LOWASA




Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakati akizungumza na
waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam amezungumzia minong’ono inayodai kwamba Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu - Bara, John Mnyika na Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria wa chama hicho kwamba walisusia tukio la Lowassa kujiunga na chama hicho.

“Jana ilipita minong’ono mingi tu, katibu mkuu wetu yupo kwenye majukumu mengi. Katika kipindi hiki cha uchaguzi tuna mambo mengi. Hatuwezi wote kuwa pamoja. Tunagawanyika kulingana na programu tulizonazo” 

No comments :

Post a Comment