Nairobi: Wakati Wadadisi wa maswala ya kidiplomasia walikuwa wamebashiri kuwa rais Obama asingelikutana naye na ima atafanya hivyo itakuwa mkutano wa kisiri wala hakutakuwa picha yoyote kwani Ruto angali anatazamwa kama mshukiwa wa makosa jinai.
Wakati huohuo , Bwana Ruto amenukuliwa mara kadhaa akikashifu hadharani swala la mapenzi ya jinsia moja. Yamkini majuma kadhaa yaliyopita, Ruto, alitangaza wazi kuwa, atapinga shinikizo za aina yoyote kutoka kwa serikali ya Rais Obama ya kutaka Kenya ihalalishe na kuwatambua watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Kulikuwa na dhana kuwa msimamo huo ungemfanya kutofautiana na rais Obama lakini hilo sasa limezikwa katika kaburi la sahau. Na alipowasili katika ikulu ya Nairobi alipokewa kwa taadhima kuu ya amiri mkuu wa jeshi na kupigiwa mizinga 21 ya heshima.
Hata hivyo hii leo Naibu Rais wa Kenya, William Ruto amekutana na Rais Barrack Obama katika ikulu ya rais nchini Kenya.
Ingawa ni salamu tu, kati ya Obama na Ruto, tendo hilo limekuwa na umuhimu mkubwa nchini Kenya na kuashiria uhusiano ulioko kati ya Kenya na Marekani.
Awali kulikuwa na tetesi kuwa wawili hao hawangekutana kutokana na kesi inayomkabili Ruto katika mahakama ya uhalifu ya ICC.
Ruto hakuwa katika wageni waliompokea Rais Obama alipotua nchini Kenya na tukio hilo lilichangia uvumi kuwa Ruto hangekutana na rais Obama.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya viliripoti kuwa Ruto hangeruhusiwa kukutana na Obama kwani ni mshukiwa kwa kuhusika katika vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini ambapo watu elfu moja waliuwawa na maelfu kuachwa bila makao.
Hata hivyo Rais Uhuru Kenyatta alieleza awali kuwa Obama atakutana na Serikali ya Kenya na Ruto ni mmoja wa viongozi wakuu katika serikali hiyo.
Kauli hiyo ilitiliwa mkazo na waziri wa nchi za nje, Amina Mohammed kwenye mahojiano ya kipekee na BBC aliposema kuwa hakuna sababu zitakazomzuia Ruto kukutana na Rais Obama. Aidha, Ruto amekuwa katika mstari wa mbele kupinga ndoa kati ya watu wa jinsia moja na kueleza kuwa Kenya haitahalalisha ndoa za aina hizo.
Takriban saa ishirini hivi tangu rais wa Marekani Barack Obama awasili nchini Kenya swala ibuka limekuwa, Je atakutana na naibu rais wa Kenya bwana William Ruto au la ?
Naibu rais Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007. Kesi dhidi yake inaendelea katika mahakama ya kimataifa ya ICC huko Hague Uholanzi.
No comments :
Post a Comment