Wednesday, July 1, 2015

SABABU NANE KWANINI WATU WANAKUNYWA SODA NA SABABU KUMI NA TANO: NI KWANINI UNATAKIWA KUACHA KUNYWA SODA

  • Na Mtaalamu wetu

Utangulizi

Wengi wetu huwa tunakunywa Soda. na wengine wanakunywa sana kuliko wengine. Hilo lipo wazi.
 Nakumbuka wakati nimepata kazi kwenye kiwanda cha SODA, mwanzoni nilikua nakunywa zaidi ya soda sita kwa siku, ingawa baadae kiwango kilipungu na kufikia walao soda tatu au nne kwa siku.
Kuna ambao hawafahamu kwamba soda ni huweza kumletea madhara mnywaji ingawa wengine wanakuwa wanafahamu lakini huwa wanapuuzia.

Nchi ya marekani ni kati ya nchi zinazo ongoza kwa matumizi makubwa ya kinywaji cha Soda. Nafikiri kunahaja ya kufahamu kwa undani kuhusu vinywaji hivi tunavyovipenda sana.

Kwanini watu wanakunywa soda?

1. Soda zina ladha nzuri
Ladha ya soda inaweza ikawa ni kivutio kikubwa kwa sisi kuzipend. Soda ni tamu na zina ladha nzuri. Hii ndiyo sababu wakati mwingine watu hutumia soda kwenye kila mlo.



2. Soda inapatikana kila mahali


Soda zinapatikana kila mahali, hata mahali ambapo hakuna mahitaji mengine ya muhimu kama vile vyakula vya msingi. Hata kama utahitaji kula vyakula vingine ni vigumu sana kuvikuta vyakula hivyo vimewekwa kwenye sehemu ilivo wazi, kwenye sehemu wanapouza vyakula au hata kwenye supermarkets.



                                               3. Urahisi wa kuchukua na kutumia.
Soda ni kati ya bidhaa rahisi sana kununua na kutumia. Urahisi huu unafanya soda kuwa option ya kwanza kwenye matumizi badala ya vinywaji vingine baridi kama juisi.





 4. Promotion na matangazo
Soda zinatumiwa sana na watu wa rika mbalimbali kwa sababu makampuni yanayotengeneza soda yanazitangaza sana bidhaa hizi. Pengine matangazo yanayosisitiza watu wanywe soda ni mengi zaidi ya matangazo yanayowasisitiza watu wale mlo kamili "balance diet". Mabilioni ya pesa huwa yanatumika kutangaza soda katika migahawa, maduka, supermarkets, vituo vya mafuta kwenye television na hata kwenye mashule.
5. Kujengeka kwa tabia
Kuna baadhi ya watu kunywa chupa kadhaa za soda kwa siku ni kitendo kinachosababishwa na kjengeka kwa hiyo tabia.
6. Ni bei rahisi
Kuna baadhi ya maeneo soda huuzwa kwa bei rahisi zaidi kuliko juisi za matunda au maziwa.
Katika baadhi ya maeneo soda hugawiwa bure baada ya kununua chakula.
7. Kukata kiu ya maji
Wakati mwingine watu hunywa soda kwa ajili ya kukata kiu. Ingawa hiki siyo kitu kizuri kwani, ukiwa na kiu kiwango cha mate hupungua kinywani, na mate ndiyo yanayohitajika katika  "ku-neutralize" kiwango acids. Sasa kama hauna mate mdomoni maana yake acid hiyo huingia moja kwa moja tumboni, na inaweza kukuletea madhara
8. Kupata Caffeine Addiction (arosto"
Vinywaji vingi baridi huwa vina chemikali inayoitwa caffeine. Caffein huweza kumfanya mtu akawa " addicted". Na hii ndiyo sababu kuu haswa inayowafanya watu wasiache tabia hii ya unywaji wa soda.

Kwanini unatakiwa kuacha kunywa soda?

Kuna sababu kubwa kumi na sita za kwanini unatakiwa kuacha kunywa soda. Je, unajua ni jinsi gani unywaji wa soda unahatarisha afya yako? Embu tuziangalie sabau zenyewe.
1. Soda hazina faida yeyote kiafya
Unatakia kufahamu kwamba soda hazina virutubisho vyovyote muhimu kwa ajili ya miili yetu. Soda zinatengenezwa kwa kutumia maji na sukari za viwanda.


       

2. Kuongezeka kwa uzito na unene
Watu wengi huwa aidha wanaisahau au hawajioni jinsi ambavyo wanapata uzito wa ziada kutokana na kunywa soda kwa wingi. Unywaji wa soda moja mil 330 kila siku unaweza kusababisha ongezeko la kilo 5 kwa mwezi. Umenipata hapo?. Wanasayansi "wame-prove" kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya unywaji wa soda na ongezeko kubwa la uzito. 
3. Kisukari
Ongezeko kubwa la uzito huweza kuongeza hatari ya kupata kisukari. Unywaji wa soda hausababishi kuongezeka kwa mafuta mwilini pekee bali hupunguza uwezo wa miili kuchakata sukari. Sukari nyingi huweza kusababisha kisukari  cha aina ya pili "TYPE 2 DIABETES"



4. ulainika kwa mifupa "Osteoporosis "
Unywaji wa soda wa mara kwa mara huongeza hatari ya kulainika kwa mifupa au kitaalamu inaitwa "Osteoporosis" . Hii husababishwa na kwamba soda husababisha upungufu wa madini ya calcium. Madini ya calcium husaidia katika kuimarisha mifupa na meno. Upatikanaji wa soda kwa wingi husababisha matumizi ya vinywaji ambavyo husaidia kuimarisha mifupa kama vile maziwa.


5. Kuoza kwa meno
Soda husababisha kulika kwa sehem ya nje ya meno au kitaalamu inaitwa " enamel erosion".
Wanasayansi wanasema unywaji wa soda vile vile husababisha juoza kwa meno
.

MUENDELEZO...
6 .Kuharibika kwa figo
Unywaji wa soda kwa wingi huweza kusababisha ugonjwa unaoitwa Figo jiwe au kwa lugha ya kigeni ni "Kidney Stone" . Vimywaji vyenye Cola ndivyo vinavyoongoza katika kusababisha matatizo ya figo zaidi ya vinywaji visivyokua na Cola.
7. Kuongezeka Pressure ya damu.
Wataalamu wanasema kwamba matumizi makubwa ya sukari, hasahasa sukari zipatikanazo kwenye Soda husababisha kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa pressure ya damu.
8. Kiungulia
Unywaji wa Soda huweza kusababisha kiungulia.
9. Matatizo katika maini
Kuna ushahidi unaonyesha kwamba matumizi ya vinywaji baridi kama Soda, huongeza hatari ya kupata matatizo katika maini.
10. Matatizo katika mmeng'enyo wa chakula.
Soda zinakiwango kikubwa sana cha acid. pH ya soda huweza kufika ata 2.1. Kiwango hichi cha pH kinaweza kuadhiri mmeng'enyo wa chakula na kufanya mmeng'enyo wa chakula usifanyike au ufanyike kwa kiasi kidogo.
"Kutokana na hili haishauriwi kunywa soda wakati wa kula chakula"
11. Kupungukiwa na maji mwilini
Soda huweza sababisha upungufu wa maji mwilini. Hii hutokea sana hasa kwenye soda zenye  "caffeine" pamoja na sukari . Chemikali hizi huchangia kuongezeka kwa kiwango cha mkojo kwa kuvuta maji kutoka kwenye mkojo kuingia kwenye mfumo wa mkojo.
" Hii ndiyo maana ukiwa na kiu  ya maji na unapokunywa soda zenye caffeine kiu ya maji huongezeka nbadala ya kupungua"
12. Soda zina kiwango kikubwa cha caffeine
Soda nyingi zina kiwango kikubwa cha caffeine. Caffein zinamadhara makubwa katika mwili kwa kusababisha kuongezeka kwa pressure ya damu, matatizo katika mmeng'enyo wa chakula, kuongezeka kwa mkoo n.k. Kwahiyo unapoacha kunywa soda utakua unajiepushia matatizo hayo na mengine mengi
13. Sukari za viwandani
Soda nyingi hutengenezwa kwa sukari za viwandani ambazo siyo sukari halisi, kwa kitaalamu zinaitwa " artificial sweetners". Sukari hizi zina zinakua na utamu mara 200 zaidi ya utamu wa asali za kawaida. Sukari hizi hutumika ili kupunguza gharama za uzalishaji.
"Nafikiri unakumbuka ishu za K.K Sukari, huo ni mfano mmojawapo wa matumizi ya artificial sweetners"
Moja ya aina ya sukari inayotumika kwa wingi ni Aspartame. Aspatame ni kati ya chemikali hatari ambayo matumizi yake yanaweza kusababisha cancer.
14. Kuharibika kwa seli hai
Wachunguzi kutoka chuo kikuu cha Uingereza wamefanya study inayoonyesha kwamba "Preservative" inayotumika sana kwenye Soda inayoitwa Sodium Benzoate inayopatikana kwenye Fanta na Pepsi inauwezo mkubwa sana wa kusababisha matatizo makubwa katika "DNA". Vile vile chemikali hii husababisha uharibifu wa seli hai na kuzifanya kuzeeka kwa haraka
15. Soda husababisha mtu kuacha matumizi ya vinywaji vyenye faida kubwa mwilini.
Kutokana na urahisi wake uipata na urahisi wa matumizi mara nyingi watu wengi hukimbilia katika matumizi ya soda na kuacha matumizi ya vyakula au vinywaji vyenye faida kubwa mwilini kama vile maziwa, juisi, chai na hata maji. Vinywaji hivi vinaumuhimu mkubwa sana kwenye afya ya binadamu .

Hitimisho

Soda ni kinywaji ambacho hakina faida yeyote katika mwili wa binadamu. Kutokana na hilo nivyema kwa watu kuwa makini hasa kwenye matumizi yake kwa kuhakikisha kwamba hawaachi matumizi ya vinywaji au vyakula vyenye faida kwa kuwa soda zinapatikana. Na kwa wale wapenzi sana wa soda ni vyema kupunguza matumizi yake kwa kuwa soda zina madhara katika afya yako.
MWISHO

No comments :

Post a Comment