Tuesday, July 21, 2015

SAED KUBENEA AJITOSA UBUNGE KUPITIA CHADEMA

                            

SAED Kubenea, ameamua kuvunja ukimya baada ya uvumi kuenea kuwa alikuwa na nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani baada ya kuchukua fomu rasmi kugombea ubunge Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam.


Akizungumza na vyombo vya habari leo mchana makao makuu ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), amesema 

“Nimeamua kugombea jimbo la Ubungo ninaamini ni demokrasia na ni haki yangu kufanya hivyo kama mtanzania” huku akizungumza kwa kujiamini kwa kurejea kauli ya baba wa Taifa, Mwl. Nyerere aliyesema wananchi wanahitaji mabadiliko, wasipoyapata ndani CCM watayatafuta nje ya CCM”.

Kwa vile wananchi wameshindwa kupata mabadiliko ndani ya CCM , Kubenea amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kupitia tiketi ya CHADEMA, chama makini, ili aweze kuwa sehemu ya Bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali kwa maslahi mapana ya watanzania na ustawi wa nchi kwa ujumla.

Alipoulizwa kuwa haoni kuwa kutakuwa na mgongano kati yake na John mnyika (MB), kwa kugombania jimbo hilo, na kama alishaomba ushauri kutoka kwa Mnyika, Kubenea amesema haoni tatizo kwani demokrasia inaruhusu yeyote mwenye sifa kugombea, zaidi ya hayo alisema sio vizuri kuongea naye kwani yeye ni Naibu Katibu Mkuu (Bara), ana nafasi kubwa ndani ya chama na yeye ni kiongozi wa wagombea wengine wote, kujadiliana naye ni kufanya ‘lobbying’, akimaanisha kufanya ushawishi kitu ambacho sio utawala bora na ni kunyima haki kwa wengine.

Hata hivyo Kubenea alisema akipata fursa atamshauri Mnyika kwenda kugombea jimbo jipya la Kibamba. Alipoulizwa endapo hataafiki kwenda Kibamba amesema ataamua kumuachia

No comments :

Post a Comment