Thursday, July 30, 2015

SERIKALI YASOGEZA MBELE DEADLINE YA KUANDIKISHA WAPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR

Tume Taifa ya Uchaguzi(NEC) imeongeza siku nne zaidi kwa wakazi jiji la Dar es Salam kujiandikisha

katika daftari la kudumu la kupiga kura ili kuwezesha watu wengi kujiandikisha.




Raisi kikwete akiandikishwa kwenye mfumo wa BVR kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo
Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dares Salaam, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema uamuzi huo umetokana na kuwepo kwa mwamko mkubwa wa wananchi waliojitokeza kwa wingi isivyo kawaida katika vituo mbalimbali.
“Tume imeamua kuongeza muda wa kulimazia watu watakaokuwapo vituoni siku ya mwisho yaani kesho tarehe 31,Julai, mwaka 2015. Sasa muda umeongezwa kwa siku nne ili kumalizi uandikishaji huo,”
Jaji aliongeza kwamba hivi sasa hadi kufikia jana tarehe 29, Julai wananchi waliojiandikisha katika daftari hilo ni 18,826,718 kwa nchi nzima , wakati lengo lilikuwa ni kufikia wananchi milioni 23 hadi 24.


Alisema hadi siku ya jana watu waliojiandikisha katika jiji hilo ni 1,754,725 sawa na asilimia 62.4, wakati makadrio ni watu 2,810,423.

No comments :

Post a Comment