Friday, August 7, 2015

CHENGE APANGUA TUHUMA 11 ZA BARAZA LA MAADILI DHIDI YAKE

Aliyekuwa Mbunge wa Bariadi Magharibi, (CCM), Andrew Chenge, amepambana na wanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwa kupinga kwa hoja tuhuma 12 zilizotolewa dhidi yake na kudai kuwa hazina ukweli na kutaka zitupiliwe mbali.

Tuhuma alizokuwa amesomewa Chenge na Mwanasheria wa Baraza, Hassan Mayunga, ni pamoja na matumizi mabaya ya ofisi alipokuwa Mwansheria Mkuu wa Serikali (AG), mwaka 1995 hadi 2005, kukiuka maadili ya viongozi wa umma, kujipatia mslahi ya kiuchumi na kutojaza katika fomu ya rasilimali na madeni.

Mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Jaji Hamis Msumi, Chenge alijitetea kuwa mkataba alioingia na Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd, ni kuwa mshauri mwelekezi anayetumia taaluma ya sheria kwa weledi kutoa huduma kama wanataaluma wengine wanavyofanya na kwamba sheria haiimzuii kufanya hivyo.

Alisema Ofisi ya AG ilishauri mikataba mitatu kati ya IPLT na Tanesco na serikali ya kuzalisha umeme na siyo Chenge na IPTL, na kwamba kutokana na umuhimu wa mikataba, Wizara ya Nishati na Madini iliandaa waraka uliopitishwa na Baraza la Mawaziri wa serikali ya awamu ya tatu ambayo haijatekelezwa hadi sasa.

Alisema waraka huo ulikubaliwa na moja ya mambo ya msingi yaliyokubaliwa ni IPTL kutumia mafuta mazito na gesi asilia ya Songosongo kuzalisha umeme, na licha ya bomba la gesi kufika Tegeta, lakini hadi sasa haitumiki kuzalisha umeme kwa kuwa utapatikana umeme wa bei rahisi na kwamba kuna ‘madudu’ mengi yamejificha.

“Kazi ya Ofisi ya AG ni kushauri mikataba yote inayoingiwa na serikali...najiuliza tena kwa mshangao nilikiuka maadili gani, walitaka nifanye nini, ninamshangao eneo hilo,” alihoji Chenge.

Alisema lalamiko la sita halina msingi wowote kwa kuwa hawajaainisha na kuorodhesha taarifa alizozipata akiwa AG na kuzitumia kwenye mkataba wake na VIP zilitumika kwa manufaa binafsi.

“Mimi ni mwanasheria mweledi, nathamini profession (taaluma) yangu, niliteuliwa kulinda na kutetea maslahi ya VIP dhidi ya Mecma na siyo vinginevyo na ili VIP alinde matarajio ya uwekezaji wa hisa asilimia 30 ndani ya kampuni ya IPTL, kubwa nilichoangalia ni 'public interest' (maslahi ya umma) na juzi nimetoka Uingereza tunailinda Tanesco na walipakodi wa Tanzania wasiletewe madai ya ovyo,” alieleza na kuongeza:

“Sijaajiriwa na VIP, ukurasa wa 11 wa mkataba unaeleza mshauri mwekelekezi wa kujitegemea na si kuajiriwa na sina manufaa kama mwajiriwa.”


“Taarifa wanazonituhumiwa nimetumia ofisi kuinufaisha VIP, sioni kokote kunakoumiza umma, serikali na Tanesco, nawataka waweke wazi taarifa zilizotokana na utumishi wangu wa nyuma, mkiwa na malalamiko kama haya hamnitendei haki mlalamikiwa na mlalamikaji hajalisaidia Baraza,” alisema.

Alisema wanahisa wa IPTL mwaka 2002 walikuwa na kesi Mahakama Kuu ya Tanzania na aliingia mkataba mwaka 2006 na kwamba hadi sasa akisoma malalamiko hayo haelewi kinachotafutwa dhidi yake.

“Mlalamikaji hajabainisha malalamiki ya mimi kuendelea kuwa mshauri mwelekezi na ubunge wangu, sheria haizuii alimradi nilinde maslahi ya umma na mkataba wake na VIP haulengi kuleta mgogoro na umma wala yeyote mwenye hisa kati ya wenye mgogoro.

Alisema tangu kuanza kazi ya ushauri makubalinao ilikuwa ni kulipwa malipo ya Sh. bilioni 1.617 baada ya mafanikio ‘success fee’ ambayo alilipwa mwaka 2014 na kwamba hana manufaa yoyyote ya kiuchumi aliyoyapata.

“Sikulipwa na VIP kwa sababu ni kiongozi wa umma bali ushauri ninaoendelea kutoa hadi sasa, mlitaka nisitumie taaluma yangu?” alihoji.

No comments :

Post a Comment