Friday, August 7, 2015

HALI MBAYA: WAFANYAKAZI WA TRA HAWAJALIPWA MISHAHARA YA MIEZI MITATU WANAYODAI

Kama wewe ni mfanyakazi nazani unafahamu machungu ya kukosa mshahara, aidha kwa kucheleweshwa kwa bahati mbaya au akusudi.Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), hawajalipwa mishahara ya miezi mitatu kati ya miezi sita waliyokuwa wakiidai mamlaka hiyo. Wafanyakazi hao hawajalipwa mishahara ya Januari, Juni na Julai, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), Patrick Nyakeke, alisema baadhi ya wafanyakazi hawajalipwa mishahara ya kuanzia Januari hadi Mei, mwaka huu.

“Wafanyakazi zaidi ya 1,500 bado hawajapewa mishahara ya miezi ya Januari, Juni na Julai huku wengine wakiwa wanaudai uongozi wa Tazara mishahara ya miezi mitano pamoja na malimbikizo mengine,” alifafanua Nyakeke.

Aidha, alisema mishahara ya Januari na Juni, mwaka huu, utalipwa na Menejimenti ya Tazara na wa Julai mwaka huu, unatarajiwa kulipwa kupitia Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ya 2015/16 iliyotengwa na serikali.

Hata hivyo, alisema baada ya wafanyakazi kuuhoji uongozi wa mamlaka hiyo kuhusu suala hilo, walielezwa kuwa watalipwa mishahara na malimbikizo ya fedha za likizo kupitia makusanyo ya Tazara ya Januari hadi Julai, mwaka huu. 

Nyakeke alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo, serikali imetenga Sh. bilioni 30 ili kuhakikisha wafanyakazi wanaondokana na adha ya kusotea mishahara.

Aidha, aliitaka serikali kuongeza vitendea kazi vikiwamo vichwa vya treni 20 kwa ajili ya kusafirisha abiria na mizigo kwani vichwa sita vilivyopo havitoshelezi kubeba mizigo mingi.

Alisema vichwa vinne hubeba tani 96 na hivyo kupata faida kidogo ambayo haitoshelezi kuliendesha shirika hilo.

Januari 15, mwaka huu, wafanyakazi wa Tazara waligoma kwa lengo la kuishinikiza menejimenti ya mamlaka hiyo kuwalipa mishahara yao.

Pia walitaka kukutana na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi kwa wakati huo, Dk. Harrison Mwakyembe, kujadili hatma ya Tazara.

No comments :

Post a Comment