Wednesday, August 5, 2015

HALI YA SINTOFAHAMU YAENDELEA CUF

Hali ya sintofahamu imeendelea kuwakumba wafuasi wa chama cha CUF kutokana na mkutano uliopangwa leo baina ya Mwenyekiti wa chama cha CUF na waandishi wa habari kuahirishwa kwa kile kinachosemekana ni wazee wa CUF kumuwekea ngumu Prof. Lipumba kuongea na waandishi wa habari.
Akiongea na waandishi wa habari Naibu Katibu wa CUF Magdalena Sakaya alisema kwamba wazee wa CUF walimzuia Prof Lipumba kuongea na vyombo vya habari mpaka wajue kwanza ni kipi Prof. Lipumba anataka kukitangaza na hivyo kuwataka wanachama kuwa na subira.
Hata hivyo baada ya muda kupita na nyimbo za wananchama wa CUF waliojazana nje ya ofisi  za CUF kuzidi Prof. Lipumba aliamua kuhairisha mkutano na wazee hao na kuamua kuongea na wanachama na kuwaambia kutoa kauli ambayo bado ilionekana kuzidi kuwavuruga wanachama hao.

No comments :

Post a Comment