Sunday, August 2, 2015

KAULI YA ZITO KABWE KUHUSU MNYIKA KUHAMIA ACT-WAZALENDO


KUMEKUWA na tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Naibu Katibu Mkuu (CHADEMA), Bara, John Mnyika, amekihama chama chake na kwenda chama cha ACT-Wazalendo.

Akizungumza issue hiyo hapa mkoani Kigoma, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo amesema hajui chochote kuhusu hilo.

Hata hivyo Zitto amesema kuwa ACT hawawezi kukataa mwanachama na kwamba yeye hana chuki na Mnyika bali zilitokea tofauti za kisiasa baina yao na kuongeza kuwa Mnyika alikuwa anatumiwa na hata yeye mwenyewe alikuwa anajua kuwa anafanya kitu ambacho sio sahihi.

Kauli hiyo ya Zitto huenda ikaendeleza mjadala juu ya Mnyika kuhamia ACT na haitashangaza kama itatokea kutokana na mazingira ya kisiasa yalivyo kwa sasa nchini.

No comments :

Post a Comment