Tuesday, August 4, 2015

MAKONGORO MAHANGA USITUZINGUE
















AGOSTI Mosi Mwaka huu ,Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiliendesha kura za maoni kwa wagombea wake kwa ngazi za Ubunge na Udiwani kote nchini. 

Kwa tuliofutilia harakati za kupatikana kwa wagombea hao kwa zaidi ya miezi mitatu sasa katika baadhi ya maeneo hapa nchini tumelishuhudia matumizi ya fedha kwa baadhi ya wapambe wa wagombea kuandaa mikutano ya wapiga kura wa CCM katika Matawi,Kata ambao walikuwa na Kadi za CCM. 

Wiki iliyopita mimi mibanfsi nilikuwa nikishinda mitaani ,kwenye vijiwe,kuzungumza na baadhi ya wanaume na wanawake ambao wengine ni wake za watu ambao ilipokuwa ikifika saa nane mchana kutwa kiguu na njia kwenda kwenye vikao vilivyokuwa vinaandaliwa na wapambe wa wagombea na wanawake hao walikuwa wakienda haraka haraka kwenye vikao hivyo vya kukutanishwa na baadhi ya wagombea kwasababu mwisho wa vikao hivyo walikuwa wakihongwa Sh.5,000, 10,000 na Sh.3,000. 

Tumesikia Madai ya tuhuma za Rushwa na uhuni wa kila aina Katika mchakato huo wa kura za maoni ndani ya CCM. 

Baada ya baadhi ya wagombea walioshinda Katika kura za maoni wametuhumiwa na wapambe wa kambi za wagombea wenzao Kuwa wametumia Rushwa na figisufigisu. 

Lakini hata Hao walioshindwa Katika kura hizo za maoni ambao wapambe wao wanalalamika Kuwa washindi walitumia Rushwa,nao pia walitumia Rushwa Katika kampeni zao kwa kuwahonga baadhi ya Wapiga kura,wajumbe wa nyumba Kumi ,mawakala wao na baadhi ya viongozi wa CCM ili wamsaidie washinde ila tu Fedha zao zimeliwa na ushindi hawajapata. 

Naomba vikao Vya juu Vya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete na Timu yake vichunguze vizuri wale wote walioshinda kura za maoni Kama walishinda kwa njia chafu basi wahenguliwe. 

Maana siyo Siri uchafu na matumizi ya Rushwa Kabla na wakati wa uchaguzi huo yalitawala katika baadhi ya majimbo na Kata vitendo ambavyo vimethibitisha Kuwa ni Ngumu sana kupata madaraka ndani ya CCM bila kumwaga Fedha na kufanya ghiriba maana Takukuru nikama walikuwa mbingu nyingine. 

Turejee Katika mada Kuu ambayo ni Agosti Mosi Mwaka huu,  aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kwa vipindi viwili mfululizo tangu mwaka 2000-2010 ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi na Ajira, Dk.Makongoro Mahanga kwa tiketi ya CCM, alishindwa katika kura za maoni . 

Agosti 2 Mwaka huu, yaani Jana Dk.Mahanga aliitisha mkutano wake na waandishi wa Habari na kutoa shutuma kuwa uchaguzi ulitawaliwa na Rushwa, hira, mizengwe na kwamba Kabla ya uchaguzi huo kufanyika Juzi . 

Mara kwa Mara alikuwa akilalamika Kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala Kuwa kuna baadhi ya wagombea wenzake wa Ubunge wanavunja Kanuni za chama lakini uongozi wa CCM Wilaya ya Ilala ulimpuuza. 

Na kwasababu hiyo ametangaza rasmi kuhama CCM anakwenda zake kujiunga na Chadema. Kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inatoa Haki ya Mtanzania yoyote kujiunga na Chama chochote cha siasa.Hivyo Kwenda kwako Chadema wala ujafuvunja Sheria za nchi. 

Siyo Siri baada ya kumsikia Dk.Makongoro Kwenye Redio na kumshuhudia Kwenye Televisheni akizungumza maneno hayo na uamuzi huo, niliishia Kusema kweli 'Mungu wa siku hizi ni kijana analipa hapa hapa Duniani' na Kwamba Muosha uwoshwa tena wakati wa kuoshwa ulipuliwa. 

Leo Dk.Mahanga analalamika Rushwa hira zimesababisha ashindwe?.Lini we Makongoro na wewe na genge Lako mliacha kucheza Michezo hiyo unayowatuhumu wenzio wamejifanya ? 

Mahanga huyu huyu ninae mfahamu Mimi anadiriki Kusema hayo?Nimecheka sana.Kweli Dk.Mahanga safari hii umempata Kiboko yako mwanamke wa Shoka Bonna Kalua ambae amekuangusha Katika kura za maoni nafasi ya Ubunge.Kalua umetoa kamasi Makongoro hadi ameamua CCM ,safi sana Kalua ,wanawake tunaweza Kuwa wabunge majimboni sio siku zote Kuwa wabunge wa viti Maalum. 

Minamuuliza huyu Bwana Makongoro huo ujasiri wa kukemea figisufisu na Rushwa Katika uchaguzi Katika Jimbo la Segerea ameupata wapi?  Ina maana ujasiri huu wa kuona Rushwa ,figisufigisu Katika uchaguzi CCM, Dk.Mahanga ameupata baada ya kubwagwa na aliyekuwa mgombea mwenzake ambaye ni binti Mdogo Juzi? 

Kweli Mtenda akitendewa uisi kaonewa na Yale yote aliyoyatenda uwa yanamrudia alijiimbiaga Mwanamuziki Ally Choki. 

We Dk.Makongoro Mahanga kweli Leo hii unapata ujasiri wa kutoa malalamiko hayo tena hadharani Wewe Huyo? 

Minimuulize Mtani wangu Dk.Mahanga Ina maana wewe na genge Lako lililokuwa likikupigia kampeni hamkutoa hata Sh.100 kwa Wapiga kura ili kuwashawishi wakipigie kura za ndiyo?  Maana wakati mwingine Nyie wanasiasa muwe mnamuogopa Mungu na muwe wa kweli. Sema Dk. Makongoro Kama kweli hukutoa hata senti Moja kwa baadhi ya Wapiga kura ili wakuchague? 

Minakufahamu vizuri sana na wewe tangu Enzi zile nakuja kuandika Habari za jimbo Lako na waandishi wenzangu ambao hivi sasa ni marehemu Jackline Mwingira(Nipashe), Agnes Yamo ( Tanzania Damia) na Veronica Charles ( Majira). 
Au Katika uchaguzi wa kura za maoni Mwaka 2015 ulishampokea Bwana Yesu ,umeokoka unampenda Yesu hivyo Figisufisu 'ghiriba' za uchaguzi wewe na kambi yako hamkuzifanya Mwaka huu? Lakini Mtani wangu wakati wewe ukiwatuhumu waliokushinda na mchakato huo Kuwa ulighubikwa na Rushwa, pia kuna Wapiga kura wa jimbo la Segerea baadhi Yao na wanakutuhumu Kuwa nawewe na kambi yako mlishiriki kucheza Michezo hiyo haramu ' Figisufisu' Katika uchaguzi huo uliomalizika Juzi. 

Ila tu uchaguzi 2010 , wana CCM Jimbo la Segerea wamekuchoka waliamua kutafuna Fedha zako kwa makusudi na Kisha KUIBWAGA na kweli wamekubwagwa kama zigo hadi umeonekana kukumbwa na kiwewe? 

Watu wamechoka za Fedha zako sasa uende nazo uko Chadema,na Chadema wameishafanya uchaguzi wa kura za maoni za Ubunge na Udiwani, sasa sijui utaweza kuvumilia Kuwa Mwanachadema wakati Huna Cheo cha Ubunge wala Udiwani? 


Maana siyo Siri kilichokuamisha CCM ni baada ya kushindwa Katika kura za maoni ya Ubunge yaani ni kukosa madaraka ndani ya CCM ndiko kulikosababisha uame CCM . Sasa ndiyo Sultani wenu Mkuu mnayemfuata huko Chadema ambaye aliamia Chadema kwa kishindo Jumanne iliyopita kwa kile alichodai aliamua kuhama CCM baada ya jina lake kuenguliwa Katika Hatua za awali za mchakato wa kumpata mgombea Urais CCM. 

Sasa Kama Chanzo cha kuhama CCM ni baada ya wewe kushindwa kura za maoni Jimbo la Segerea, umeamua kuhamia Chadema, sasa kwakuwa wewe mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa mmeonyesha Kuwa Shida yenu Kuu ni Kupata madaraka tu . Ikitokea Chadema wakakunyima madaraka siutaihama Chadema kwa Kigezo Kuwa hawajakupa madaraka? 

Tamaa na Kupenda madaraka itakuja kuwadhuru siku Moja.Yaani mjue mnawashangaza sana watu wanaofikiri sawa sawa. Dk.Mahanga ,waziri mzima umekaa Katika baraza la Mawaziri Katika serikali ya awamu ya nne yote Kama Niabu Waziri eti umeshindwa kura za maoni basi bila haya wala hujui vibaya unasema Rushwa ilitawala Katika uchaguzi na kwamba unahama CCM. Unamdanganya nani na unamkomoa nani? 

Mimi nimekuwa nikikufuatilia nyendo zako muda mrefu kisiasa wewe Makongoro ulikuwa Team Lowassa na siyo dhambi.Na ni mbunge ambaye Wapiga Kuwa wa Jimbo la Segerea walikuwa wameishakukinai na Ndio maana wamekubwaga. Mpango wenu wa kitoto wa kuhama CCM Kama aliyekuwa mgombea wenu wa urais jina lake lisipopitishwa na CCM Kuwa mgombea urais, ule hajulikani NA watu wenye akili timamu . 


Watu wakawa wanawatazama nakuwaacha mjazane Ujinga, matumaini makubwa ya kupeana madaraka na mtekeketeze fedha zenu sasa mgombea wenu alipokatwa jina na vikao Vya juu vya CCM Dodoma ndiyo kambi yenu mkaanza kupata wazimu Msijue pakukamata maana mkijiamini sana na Fedha nyingi mkateketeza na mlilolitaka hamkulipata. 

Sisi wajuzi wa mambo ulipotangaza Jana unahama CCM ,tuliishia kucheka na kukuonea huruma tu Manaa Miaka yote mlivyoenda Timu Lowassa mlifikiri mmejificha Kwenye Giza Kumbe mlijificha Kwenye Mawingu mnaonekana,watu wana Wachora wanajua wanawakona wapi.Na ndiyo basi Mtani wangu Ubunge na unaibu waziri umeutema. 

Waswahili wanamsemo wao usemao " Aliyejamba atakunya tu". Siku zote ulijidai ni CCM Damu na upo na CCM Katika Shida na raha lakini Juzi baada ya kushindwa Katika kura za maoni ( Ndio wakati wa Shida), umeamua kuitosa CCM na kwenda Chadema mchana kweupe .Balaa. 

Licha ni Haki yako ya Kikatiba kuamia Chama chochote unachotaka. lla Mimi Kama Mtani wako nakwambia hivi uamuzi wako wa kuamia Chadema hautakuwa na faida kwako zaidi ya Majuto muda Si mrefu,tusubiri Tuone na hili litatokea usije kulia na Mtu. 

Leo Dk.Mahanga Unaiona Chadema ni nzuri na umeamua kujiunga nayo wakati mi nakumbuka ni hawa hawa Chadema ndiyo walikuwa wakikutukana matusi usiku kucha Katika mitandao na magazeti Kuwa wewe ni "Fisadi wa Elimu" , umeghushi Vyeti Vya elimu . 
Na kwamba Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 hukushinda, ulimuibia kura aliyekuwa Mgombea Ubunge (Fredy Mpendazoe)? 

Na kila ulipopita walikuwa wanakuchafua hasa na hadi siku ile Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara,Dar Es Salaam,ulioposhinda Kesi ya kupinga Bunge wako iliyokuwa imefunguliwa na Mpendazoe dhidi yako na wenzako?Kesi ya kupinga Ubunge wako na zile Kesi zote za kudhalilishwa na Kaineruba. 

Lini Chadema wamekusafisha wewe? Mtani wangu Mahanga sio kila siku lazima uwe Mbunge ,Naibu waziri. Siku nyingine Unatakiwa uwe Mwananchi wa kawaida na wewe watu wakuongoze.Mahanga acha kutuzeveza. 


Tamaa ya madaraka itakuja kuwawaisha Kuzimu maana unaweza kujikuta unaanguka ghafla na kufariki kwa BP baada ya kupata taarifa umeshindwa Katika uchaguzi uliokuwa ukigombea.  Nakushauri wewe na wenzio ambao ni wazi mna onyesha mnapenda sana kupata madaraka nendeni katika makanisa ya Kiroho mkakemewe hili hiyo roho ya Kupenda madaraka iwatoke. 


Maana hiyo roho ya Kupenda madaraka inawasumbua ,kuwatesa na kuwadhalilisha sana .Na Kwa Mungu hakuna linashindikana. Mtani wangu Hupaswi Kulalamika Katika uchaguzi huu ulioshindwa eti uligubikwa .Na figisufigisu, inakupasa ukae chini ujiulize ni kwanini hizo figisufigisu unazodai zilikuwepo zikasababisha ushindwe ni kwanini zimetokea na ni kwanini wewe kambi yako na mawakala wako ,mamlaka husika mlishindwa kuthibiti figisufigisu hizo unazodai zilishamiri? 


Uoni figisufigisu hizo ni malipo kwako kutokana na figisufigisu ulizotuhumiwa kumfanyia aliyekuwa mgombea Ubunge (Chadema) Mwaka 2010 ? Watoto wa mjini tunasema " Malipo ni Dunia akhera kuhesabiwa usijigeuze nyani kucheka uliyoumbiwa". Sasa basi figisufigisu zilizokupaa Katika kura za maoni CCM Juzi ni malipo ya figisufigisu zile. 

Minawashauri watu walionizidi umri,na viongozi wetu Nyie msipende kuchukua maamuzi wakati mnahasira na machungu moyoni Kwani mwisho wa siku mtajikuta mnajutia maamuzi hayo mliyoyachukua wakati mnahasira na uchungu moyoni. 


Mtani wangu Mahanga Nakutakia kila lakheri katika makazi mapya ya siasa huko ulikosema anaenda kuamia Chadema, Mungu akutangulie.Ila tabia ya kuama Chama na kutoa kashfa dhidi ya CCM baada ya kushindwa kura za maoni uache haitokufikisha Kokote Kwani hata huko uendako Kama kuna viongozi wenye akili timamu na wenye busara wana Haki ya kukataa usijiunge na Chama chao kwasababu kupitia maelezo yako ni wazi unaamia Chadema siyo kwasababu unaipenda Chadema kutoka moyoni. 


Unahama Chadema baada ya kushindwa Katika kura za maoni za Ubunge CCM Juzi, na Jana ukatangaza unahama CCM unaenda Chadema. Hivi nikikuuliza wewe Dk.Mahanga lini ulijipa muda ukaisoma Katiba ya Chadema na Kanuni zake ukazielewa vyema na zikakuvutia ndani ya saa 24 ukaamua kujiunga na Chadema? 

Chadema muwe makini sana na hili Wimbo la makada wa CCM waliokosa fursa za uongozi ndani ya CCM wanaamua kujiunga na Chadema. Kuweni nao makini sana, Wengi wao wana uchu na tamaa ya madaraka na viongozi wa aina hii mnavyozidi kuwakaribisha misiwakatazi msiwakatibishe ila Mkae mkijua hipo siku watawasumbua. 

Mwenye Kilema abadili Mwendo. Lowassa,Dk.Mahanga tayari wameisha jidhihirisha ni aina ya binadamu wanaopenda madaraka kupita kiasi.Hivyo licha wamekuja Chadema Lowassa mmempa nafasi Adimu ya Kuwa mgombea urais ambayo nafasi hiyo Ina malizika Oktoba 25 Mwaka huu . 


Fedha na mali wanazo lakini wanachokisaka kwa kwa udi na uvumba ni madaraka.Watu wenye akili timamu na tunaofikiri sawa sawa tu nawaogopa sana sana. Mimi binafsi naamini Lowassa hawezi Kuwa rais kupitia Chadema.Huo ndiyo ukweli mchungu nafahamu itawakera sana Chadema na baadhi ya watu wa Kanda ya Kaskazini ambao huku mitaani hivi sasa wanasema wanaeneza siasa za ukanda wa Kaskazini lakini vumilieni. 

Swali Je, Cheo hicho cha ugombea urais wa Chadema ambacho anacho Lowassa kwa sasa kikimalizika Oktoba 25 Mwaka huu. Je Mzee wangu Lowassa atavumulia kuishi Chadema bila kupewa Cheo chochote kikubwa ? Kweli nimeamini wanasiasa Wengi ni walafi wa madaraka,hawajui kukosa ,wanajua kupata tu siku zote. CCM Kwao uwa ni nzuri pale inapowapa madaraka lakini CCM hiyo ugeuka Kuwa Mbaya Kwao pindi anapokosa madaraka au Kama wanapoona kuna Dalili za kushindwa Katika uchaguzi wa CCM. 

Ndiyo Lowassa na Mahanga,Ester Bulaya, James Lembeli CCM ni Mbaya kwasababu wamekosa madaraka ila Kipindi kile wana madaraka ndani ya CCM , walikuwa wakitamba majukwani kuwa CCM ni Chama bora na Hakuna Kama CCM na hawatahama CCM . 

Mei Mwaka huu, Lowassa Katika mikutano yake na waandishi wa Habari ambayo imerekodiwa alijiapiza kuwa Katu hawezi kuhama CCM hata kidogo. Miuwa nawasikitikiaga sana watu wa aina hii na kuwaombea kwa Mungu awatengeneze upya kiroho. 

Itakumbukwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ,Julai 28 Mwaka huu, wakati akihutubia umma Katika mkutano wa kumkabidhi rasmi Kadi ya Chadema, Lowassa,pamoja na mambo mengine Mbowe alinukuliwa akisema Kuwa alitumia Miezi mitatu kufanya mawasiliano na Lowassa ya kumshawishi Lowassaa ajiunge na Chadema. 

Wenye akili timamu tumeitafakari hiyo Kauli ya Mbowe Kuwa alitumia Miezi mitatu kufanyamawasiliano na Lowassa ajiunge na Chadema na kweli Chadema umefanyikiwa kumnasa mgombea Lowassa Julai 10 Mwaka huu, CCM ndiyo ilichuja Majina ya wagombea urais ikiwemo jina la Lowassa kwa kuyakata na kupata tano bora ambapo Lowassa akufika tano Bora. 

Ndani ya Miezi hiyo mitatu aliyotueleza Mbowe, Lowassa alikuwa ni miongoni mwa wagombea urais kwa CCM na ni wazi CCM ilikuwa ikiwafuatilia nyendo za wagombea wake wote kwa karibu. 
Ikiwa Hali ndiyo ilikuwa baina ya Lowassa aliyekuwa mgombea urais CCM alikuwa na mawasiliano Mwenyekiti wa Chadema ,Mbowe ili Lowassa aame CCM.Mnafikiri wanausalama wa CCM walikuwa hawajabaini Njama hiyo chafu ya Lowassa ya kusaliti CCM kwa Chadema? 

Kama CCM walibaini mawasiliano hayo ya Lowassa na Mbowe ya kuhama CCM hatuoni nayo hiyo ni miongoni mwa Sababu uenda zilizotumiwa na Kikao CCM kumuhuengua Lowassa mapema Katika kinyang'anyiro cha ugombea urais CCM? 

Minafananisha hiyo alilolisema Mbowe Kuwa alikuwa akimtongoza Lowassa ili aamie Chadema, ni sawa Mke wa Mtu Aliyepo ndani ya ndoa ila kwakuwa tu ni Malaya Akaamua Kuwa anasaliti ndoa yake kwa bwana mwingine.Maana huwezi Kuwa Mke wa Mtu au mume wa Mtu halafu ukaanza kutongozwa Mara kwa Mara na bwana mwingine ukakubari wakati ukijua una ndoa yako,ukifanya hivyo ukae ukijua jina unalostahili kupachikwa ni mwanamke au mwanaume Malaya. 

Maana haiwezekani uwe mgombea urais CCM mwenye hadhi ya madaraka aliyowahi kushika Lowassa ambaye hadi sasa analindwa na walinzi waliokula kiapo cha kutii serikali iliyopo madarakani na Amir Jeshi Mkuu ,halafu uwe unafanya mipango ya kuhamia Chama cha upinzani halafu vyombo Vya Ulinzi na Usalama visibaini Usaliti huu. 

Vilibaini Njama yake hiyo mapema vikawa vinamtazama kwasababu Tayari walikuwa wanajua wakati wanaoutaka wao utafika na watamtia adabu, na kweli adabu waliomshikisha kwa Kulikata jina lake mapema bila kuogopa Kuwa anaungwa mkono na baadhi ya watu. 

Chadema Mnapaswa mjiulize Lowassa huyu ambaye ndiye mgombea wenu wa urais wa sasa Enzi zile alipokuwa mgombea wa CCM aliweza kurubuniwa na Mbowe ili aamie Chadema na kweli amerubunika baada ya CCM kuchinja jina lake Kahamia Chadema, hamuoni huyu mgombea wenu wa urais Lowassa akitokea Mtu mwingine amshawishi aihame Chadema anaweza kuhama? 

Mungu Ibariki Tanzania

Imeandikwa na Happiness Katabazi
0716 774494
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
3/8/2015.

No comments :

Post a Comment