Sunday, August 2, 2015

UCHAGUZI WA KATA CCM-VIGOGO HALI MBAYA





Mwigulu Nchemba akipiga kura ya Maoni ya kumchagua Mbunge na Diwani atakayewakilisha Wananchi Wilaya ya Iramba. 
Matokeo ya awali ya kura za maoni kwa wagombea udiwani na ubunge kupitia Chama
cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi uliofanywa jana katika baadhi ya kata yameanza kutangazwa huku baadhi ya vigogo wakiangushwa vibaya.

Baadhi ya majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam, yamekuwa na upinzani mkali, ambapo aliyekuwa Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga na Jimbo la Ukonga na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, wameanguka vibaya. Katika matokeo hayo Jimbo la UKONGA: Anayeongoza ni Ramesh Patel kwa kupata kura 5139 dhidi ya Jerry Slaa aliyepata kura 1034.

SEGEREA: Bona Kalua anaongoza katika kura za awali na kumuangusha aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.

ILALA: Mbunge aliyekuwa anaongoza jimbo hilo Mussa Azzan Zungu anaongoza katika kura za awali

KINONDONI: Idd Azzan anaongoza katika matokeo ya awali

UBUNGO: Dk. Didas Masaburi

Mwanahabari mkongwe Saed Kubenea anayegombea ubunge jimbo la Ubungo, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),ameibuka kidedea katika kura za maoni kwa kujizolea kura 61 akifuatiwa na Goodluck Mollel kura 20 na Gudat Lehad akiambulia kura nne.

CHALINZE: Ridhiwan Kikwete ameongoza kata kumi kati ya 15.

KIBAHA VIJIJINI: Hamoud Jumaa ameongoza kata nane kati ya 11.

BAGAMOYO: Dk. Shukuru Kawambwa ameongoza kata sita kati ya tisa.

KIBAHA MJINI: Silvestry Koka anaongoza kata tisa kati ya 14.

TANGA: Salum Kisauji (4240), Omary Nundu (3684), Kassimu Mbughuni (1218), Kassimu Makube (1082), Athuma Baruani (948). Matokeo hayo ni ya kata 16 bado kata 11.

KOROGWE: Kata ya Majengo ni Mary Chatanda anaongoza kwa kura 238, akifuatiwa na Francis Bago (83), Yussuph Nassir 21 na Mustapha Berko 12.

KOROGWE VIJIJINI: Kata ya Mnyuzi Stephen Ngonyani 30, Dk Edmund Mndolwa, 30, Ernest Kimaya 10, Cecilia Korassa 4, Allly Hozza 4.

PANGANI: Kata ya Pangani Magharibi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Jumaa Awesso anaongoza kwa kura 479, Abdulrahaman Magati 300, Salehe Pamba 270.

BUMBULI: January Makamba amepata kura,13,366, Kaniki kura 1,781, Mshihiri kura 171, Shekwevi kura 46 huku kura zote zilizopigwa zikiwa ni 15,364.

MOROGORO: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Utumishi) Celina Kombani,ambaye ni Mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Ulanga Mashariki ameshinda katika mchujo wa kura za maoni.

Kombani aliwashinda wapinzani wake Agustino Matefu na Daud Kitolelo kwa kuongoza kwa kura nyingi katika vituo vyote 123.

MOROGORO MJINI: Mbunge Mtetezi wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameelekea kushinda tena baada ya wanachama kumpigia kwa nyingi katika Kata 29 za manispaa hiyo.

Katika uchaguzi huo anachuana na wagombea wawili akiwemo Simon Barege , na Peter Ongara ambaye imeelezwa tayari alishajiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.

DODOMA: Tawi la Chinyoya ndani ya Kata ya Kilimani: Anthony Mavunde alipata kura 91 akifuatiwa na Dk.David Malole, aliyepata kura 13.

Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano, Haidary Guramali (34), Mloki Alexander Mloki (0), Robert Mchami (1), Anthony Kanyamakura (3), Emmanuel Kamara kura (2), Mohamed Ngori (0), Musa Luhamo (0) na Steven Masangia (15).

Matokeo ya awali ya kura za maoni za kusaka ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapindzuzi (CCM) katika majimbo yaliyopo baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa.

NYAMAGANA: Stanslaus Mabula

MUSOMA MJINI: Vedastus Mathayo

MUSOMA VIJIJINI: Sospeter Muhongo

BUTIAMA: Nimrod Mkono

RORYA: Lameck Airo

MWIBARA: Kangi Lugola

KAHAMA: Katibu wa CCM wa wilaya Alexandrina Katabi, alisema matokeo yote ya watia nia ya ubunge katika majimbo yote yaliyopo wilayani humo, yatatangazwa asubuhi leo.

Hata hivyo, katika hatua nyinngine wanachama zaidi ya 70 wa CCM wilayani humo, waliandamana na kuchana kadi zao na wengine kuzirudisha kwa madai ya kutoridhishwa na mchakato mzima wa upigaji kura.

BUKOMBE: Dotto Mpira alikuwa akiongoza kura za awali

GEITA VIJIJINI: Joseph Kasheku Msukuma alikuwa akiongoza

BUCHOSA: Charles Tizeba alikuwa akiongoza

NYANG'WALE: Hussein Nassor Amar

MBOGWE: Augustine Masele

SENGEREMA: William Ngeleja alikuwa anachuana na Lawrance Masha

GEITA MJINI: Costantine Kanyasu alikuwa anaoongoza

JIMBO LA MTAMA:Nape Mnauye karibu kata zote amejinyakulia kura nyingi dhidi ya wapinzani wenzake watano.

LUDEWA: Deo Filikunjombe katika matawi 13 ameongoza na kuwaacha wagombea wenzake mbali baada ya kupata kura 2933

KISARAWE: Seleman Jafo ameongoza kata 14 kati ya 16.

KALENGA: Mwingulu Nchemba

MULEBA KUSINI:Profesa Anna Tibaijuka

MOSHI VIJIJINI: Dk. Cyril Chami (5563), anayemfuatia ni Ansi Mmas (3176)

MWANGA: Profesa Jumanne Maghembe anaongoza kwenye kura za awali.

SENGEREMA: Ngeleja amepeta na kumshinda Lawrence Masha

MUFINDI: Cosatho Chumi ameongoza na kumuangusha Naibu waziri wa maliasili na Utalii Mahamoud Mgimwa .

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment