Thursday, August 6, 2015

WATATU MBARONI KWA MAUAJI YA POLISI

Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika
na mauaji ya ofisa wake Marehemu ASP Elibariki Palangyo (Pichani) huko Yombo Kilakala Dar es Salaam.

Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro alise tukio hilo la mauaji lilitokea Agosti 4, mwaka huu nyumbani kwa marehemu.

Kamanda Sirro, amesema kua Polisi Mkoa wa Temeke ilifanya msako mkali dhidi ya watuhumiwa wa tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wa tatu wanaosadikiwa kuhusika na mauaji hayo.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kua ni Salim Khatib (32) dereva bodaboda Mkazibwa Tabata Luis aliyekamatiwa maeneo ya Kiwalani akiwa mafichoni. Mtuhumiwa mwingine ni Ismail Said (36) dereva bodaboda na mkazi wa Yombo Makangarawe, pamoja na Pirimini Haulemi (25), dereva bodaboda mkazi wa Yombo Makangarawe.

Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali ilikuweza kubaini watuhumiwa wote waliohusika katika mauaji hayo.

Aidha Kamanda Simon Sorro ametoa wito kwa raia wema kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa sahihi na za uhakika zitakazosaidia kupatikana kwa watuhumiwa wa tukio hilo la mauaji pamoja na matukio mengine ya uhalifu.

No comments :

Post a Comment