Wakati chama cha ACT- Maendeleo kikiendelea kujizolea wanachama, aliyewahi kuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Khalid Kagenzi naye alionekana katika ofisi za ACT-Maendeleo.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kama amehamia Kagenzi alijibu:
“Ni haki ya kila Mtanzania kujiunga na chama chochote cha siasa anachokitaka. Bado sijachukua kadi yangu ya uanachama,”
Kagenzi alikuwa ni mlinzi wa Dr. Slaa kwa takribani miaka 14, ambapo kibarua chake kiliingia matatani mara baada ya kutuhumiwa kutaka kumuua Dr. Slaa kwa sumu aliyopewa na viongozi wa CCM.
Kama unataka kujikumbusha zaidi, Bonyeza HAPA
No comments :
Post a Comment