Friday, July 31, 2015

Burundi:Agathon Rwasa ni naibu wa spika

Bunge lipya lililochaguliwa nchini Burundi limewateua viongozi wake.Licha ya kupinga
uchaguzi mkuu wa hivi majuzi kiongozi wa upinzani Agathon Rwasa amekubali kuwa naibu wa spika.
Wadhifa wa spika umekabidhiwa mwenyekiti wa chama kinachotawala CNDD FDD Pascal Nyabenda.
Rwasa alijipatia kura 108 kati ya kura 112
Baada ya uteuzi wa leo, imebainika wazi kuwa uongozi wa bunge hilo utatawaliwa na wanaume kutokana na kuondolewa sheria ya ndani walioweka kuwa lazima kuwe na uakilishi wa wanawake japo mmoja, katika uongozi wa bunge hilo.
Rwasa alijipatia kura 108 kati ya 112 baada ya kupata uungwaji mkono na chama cha CNDD-FDD.
Zaidi ya watu 70 walipoteza maisha yao baada ya makabiliano kati ya wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza na wapinzani waliomtaka asigombee kiti muhula wa tatu wa urais.
Wapinzani walidai kuwa muhula huo unakiuka sheria za nchini.
Naye rais Nkurunziza alishikilia kuwa muhula wa kwanza hakuchaguliwa na watu ,kwa hivyo haikuwa kinyume na sheria kwake kuwania muhula mwengine wa urais.

No comments :

Post a Comment