Utangulizi
Utangulizi
Kwamujibu wa Jarida la Habari za Matibabu (Medical News Today); Hangover ni mkusanyiko wa dalili ambazo huusishwa na unywaji wa pombe au vileo, ambao umetokea karibuni. Maranyingi hangover hutokea mara baada ya masaa 24 baada ya kunywa pombe. Mtu mwenye hangover hupata dalili mbalimbali kama vile kuumwa kichwa, kujisikia mgonjwa, kizunguzungu, kujihisi kuchanganyikiwa kujihisi kiu ya maji, n.k.
Hangover inawezekana ikatokea mda wowote, lakini mara nyingi hutokea wakati wa asubuhi mara baada ya usiku wa kula "gambe".
Licha ya dalili ambazo mtu anazipata na kuzikia mwilini mwake, vilevile hangover humfanya mtu ajisikie hali ya msongo wa mawazo, kujuta, aibu na hata hali ya kujihisi ameaibika au aibishwa.
Nini kinasababisha hangover?
Kwa mujibu wa Professor Oliver James, Mkuu wa Idara ya Matibabu chuo kikuu Newcastle University, pombe huzuia utengenezwaji wa homoni inayoitwa "vasopressin", homoni hii hudhibiti kiwango cha maji kinatolewa na figo nje ya mwili kupitia mkojo. Upungufu wa homoni hii hufanya maji mengi kutolewa nje ya mwili, na ndiyo sababu ya watu kukojoa kwa wingi wanapokunywa pombe. Kila lita moja ya pombe hufanya ongezeko la ml 10 za mkojo
.Kiwango cha hangover kinategemeana na kiwango cha unywaji au kiasi cha pombe kilichonywewa. Sababu zingine ni muda mtu alitumia kulala. Kama mtu atalala kwa mda mfupi ndivyo atakavyopata " hangover" kwa kiasi kikubwa. Ni vigumu sana kusema ni kiasi gani cha kileo mtu anapaswa kunywa ili asipate "hangover"-suala hili linategemeana na mtu mwenyewe; kwa maan kwamba itategemeana na huyo mtu alikua kwenye hali gani kabla ya kuanza kunywa au kupata kileo. Je, Alikua amechoka kiasi gani kabla hajanza kunywa, alikua na kiasi gani cha maji mwilini kabla hajaanza kunywa, Je alikunywa maji kabla hajanza kupata kileo (vileo) na wakati wa kunywa pombe.
"Kutokana na hili vi vyema kwa mtu kuanza na maji kabla ya kuanza kusukumizia bia au vileo vingine, na vilevile ni muhimu mtu kunywa maji mengi baada ya kunywa au katikati ya "gambe", hii ni kwa sababu unywaji wa maji utasaidia kurudisha maji yaliyopotea mwilini kutokana na kupata haja ndogo mara kwa mara"
Dalili za hangover
Dalili kubwa za hangover ni kuumwa kichwa au kujihisi kiu ya maji.
Dalili za hangover huanza kutokea pale kiwango cha kileo au pombe kinapoanza kupungua kwenye damu, mara nyingi hali hii hutokea baada ya masaa 24. Kwahiyo itategemeana na mtu alianza kunywa bia au vileo vingine saa ngapi.
Dalili zingine za hangover mi kama zifuatazo;
Dalili zingine za hangover mi kama zifuatazo;
- Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
- Mwili na misuli kuuma
- Kuharisha
- Kizunguzungu
- Kupumua kwa shida
- Kutokwa na mate mengi
- Kutoa "hewa chafu"
- Kichefuchefu
- Kuwa "sensitive" sana na kelele
- Kuumwa tumbo
- Kupoteza mudi "moodiness"
- Kukosa usingizi
- Kupata kiu
- Kutapika
- Kupungua kwa joto la mwili
- Mtu kupoteza "network"
- Mtu kupata msongo wa mawazo "Depression"
Jinsi ya kuondokana na hangover
Jinsi ya kuondokana na hangover
kwa mujibu wa jarida la afya- Health.com njia sahihi ya kuondokana na hangover ni kunywa pombe "kistaarabu" au kuacha kabisa kunywa pombe au vileo.
Njia zingine zinazoweza kutumika ni kuhakikisha unapata maji ya kutosha au kunywa kinywaji kisichokuwa na kileo kila baada ya bia moja au bia kadhaa na kula vyakula vyenye mafuta ili kupunguza kasi ya pombe kuingia kwenye damu au mwilini.
"Nyama choma kwa wingi, ama nini"
Unywaji wa maji husaidia kurudisha mwilini maji, kwani chanzo kikubwa cha hangover ni mwili kuishiwa maji .
"Kwahiyo ukimuona mtu anakunywa maji kila baada ya bia kadhaa usifikiri kwamba hana ela ya bia, mwenzako amegundua siri"
Njia nyingine zinaweza kutumika lakini kuna baadhi ya njia zinafanya kazi na zingine huwa hazitoi matokeo ya kweli na wakati mwingine huzidisha hangover.
Baadhi ya njia ambazo watu wengi wanazitumia ni hizi zifuatazo;
Njia hii hutumiwa sana na watu wakiamini kwamba kitendo hicho huondoa hangover.
Kitaalamu kitendo hichi hakiondoi hangover bali huituliza kwa mda Kama tulivyogusia hapo awali, mtu huanza kuzipata dalili za hangover pale kiwango cha pombe kinapoanz kushuka kwenye damu, kwahiyo unapokunywa bia zingine utakua unaongeza kiwango cha alcohol kwenye damu hivyo kuzisimamisha kwa mda dalili hizo. Dalili hizo huweza kujirudia baada ya masaa au siku kulingana na kiwango cha pombe ulichokunywa na kuifanya hali kuwa mbaya zaidi.
2. Kupata kifungua kinywa chenye asili ya mafuta kama supu
Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba vya ulaji wa vyakula vyenye mafuta hukata hangover ingawa watu wengi wanatoa ushahidi kwamba supu na nyama hukata hangover. "Wakati mwingine vyakula vyenye mafuta huishia kuwaasababishia watu kiungulia" anasema Dr. Cutler. A nashauri ulaji wa vyakula ambavyo ni rahisi kufanyiwa mmeng'enyo na mwili kama vile vyakula vinavyotokana na nafaka ambavyo anasema husaidia katika kuurudishia mwili nguvu iliyopotea. Mwanasayansi mwingine , John Brick, PhD, ambaye ni mtafiti wa vileo na mwandishi wa kitabu kinachoitwa "The Doctor’s Hangover Handbook" anaamini kwamba kula kidogo na kunywa maji mengi husaidia katika kurudisha maji mwilini nakukata hangover. Anaamini kwamba hakuna vyakula maalumu kwa ajili ya kukata hangover ingawa anamaini sandwiches zenye asali husaidia baadhi ya watu. Ushauri mwingine ni kula matunda kama vile ndizi na apple. Matunda haya yana kiwango kikubwa cha sukari ambayo itasaidia kukurudishia nguvu ulizopoteza. Vile vile matunda haya yana madini kama vile potassium na magnesium. Magnesium hutumika katika kuusaidia mwili " ku-relax" na kusaidi kuondokana na kichefuchefu3. Kutumia kahawa
Wakati mwingine watu hunywa kahawa ili kukata hangover. Wanasayansi wanasema kwamba matumizi ya kahawa husisimua mwili hivyo husababisha mwili kuhitaji nguvu za ziada. Si hivyo tu pia na mishipa ya damu kusinyaa na kuongeza presha ya damu kitu ambacho husababisha maumivu ya kichwa hivyo kuongeza makali ya hangover.
Hali hii huweza kutokea kwa wanywaji wa "Energy drinks" ambapo kinachotokea mwili husisimka na kuufanya uzalishe kiwango kikubwa cha nguvu " energy" zaidi ata ya kile kiwango kinacholetwa na hivyo vinywaji.
Njia ya rahisi na sahihi ni kunywa chai iliyochanganywa na limao kikombe kimoja au viwili "usizidishe kwani inaweza kukufanya utokwe na haja ndogo nyingi hivyo kukuletea shida tena ya kupungukiwa na maji"
4. Kufanya mazoezi
Kama mtu anajiweza ufanyaji wa mazoezi unaweza kusaidia kurudisha mwili katika hali yake ya kawaida. Ingawa kwa mtu aliyekunywa pombe kufanya mazoezi baada ya kuamka siyo jambo la msingi, cha msingi zaidi ni kupata mda wa kutosha wa kupumzika
5. Kuoga
Kuoga ni njia mojawapo inayoshauriwa na wataalamu katika kupunguza hangover. Kuoga huusaidia mwili ku-relax . Joto la maji litategemeana na mtu atakavyopendelea kwani maji ya baridi husaidia kuamsha mwili wakati maji ya moto husaidia kuufanya mwili na misuli kurelax. Kwaiyo kama una-system nzuri ya maji unaweza "ku-altenate" kati ya maji ya moto na baridi.
Maji ya moto sana au mvuke kwa wenye sauna haishauriwi kwani kitendo hicho husababisha kutanuka sana kwa mishipa ya damu na hivyo huweza kuleta shida katika mzunguko wa damu. Watafiti kutoka kampuni ya Utafiti inayoitwa Finnish State Alcohol iliyopo Helsinki, wanataadharisha matumizi ya Sauna kwamba ni hatari kwa afya, kwani yanaweza sabaisha kushuka kwa presha ya damu na mabadiliko katika mapigo ya moyo kutokana na kutanuka kwa mishipa ya damu.
6. Kulala
Kupata muda wa kutosha wa kulala ni njia moja wapo inayopendekezwa na wataalamu katika kupunguza machungu ya hangover. Mara nyingi mtu anapokuwa amekunywa sana, kulala kwake kunakuwa ni kwa taabu, anaweza akalala mwanzoni lakini baada ya muda usingizi huweza kumuishia na au kuanza kushituka mara kwa mara. Kwahiyo kama siku itakayofuata utapata muda wa kulala na ukalala "mwili wako unaweza ukakushukuru"
Hitimisho.
Kuna njia nyingine nyingi zaidi ya hizi nilizotaja ambazo zinaweza kutmiwa na watu katika kuwaondolea maumivu ya hangover. Cha muhimu ni kuchagua njia sahihi na kufuata ushauri wa kitaalamu kwani njia nyingine zikausababishia mwili madhara kiafya.
No comments :
Post a Comment