Tuesday, July 21, 2015

JE, NI KIASI GANI CHA MAJI UNAPASWA KUNYWA KWA SIKU

                       


Kadiri joto linavyopanda ndivyo ambavyo watu wanakunywa maji mengi ili kuifanya miili isiishiwe maji. Wakati mwingine watu wanashauri kwamba mtu anatakiwa kunywa hadi glasi nane wa siku. Ingawa ushauri huu hautokani na uchunguzi wa kisayansi na madaktari wanashauri kwamba inawezekana ushauri huo usiwe ndiyo ushauri bora zaidi.
Makala mpya iliyochapishwa katika Jarida la  Harvard Health Letter inashauri watu kunywa
 lita 1 mpaka lita 1.5 kwa siku, sawa na glass nne hadi sita.
Kunywa maji ya kutosha ni muhimu sana katika kusafirisha virutubisho kwenda kwenye seli hai, kuzuia mwili kuishiwa maji hasa majira ya joto,  na kuondoa sumu mwilini. Maji mengi huitajika zaidi kwa watu wanaofanya mazoezi, au wanawake wajawazito au wanaonyonyesha.
Maji pekee yasiyoongezwa kitu kama vile sukari ni chaguo zuri zaidi. Wakati mwingine maji hupatikana kwenye mchanganyiko wa vinywaji vingine.
Vyakula vingine kama vile tikitimaji na matunda mengine huweza kuongeza kiwango cha maji mwilini tunachokichukua kwa siku.
Wataalamu wa afya wanashauri kwamba "usidharau kiu yako" kwani hiyo ni dalili kwamba mwili wako unaupungufu wa maji.
Kwa mujibu wa WebMD, dalili zingine za upungufu wa maji ni kama, kuishiwa nguvu, kizunguzungu, kuzirai, n.k. Rangi ya mkojo vilevile huweza kuonyesha kwamba mwili unaupungufu wa maji. Iwapo mkojo unarangi ya ya njano iliyokolea hiyo ni dalili kwamba kunaupungufu wa maji.

No comments :

Post a Comment