Wednesday, July 29, 2015

KATIBU MKUU WA CCM DODOMA 'ALBERT MGUMBA' ATISHIA 'KUYAKATA' MAJINA YA WATIA NIA

Mbunge wa Jimbo la Mtera na mtia nia wa jimbo hilo, Livingstone Lusinde
Livingstone Lusinde-Mbunge wa Jimbo la Mtera
KATIBU wa CCM mkoa wa Dodoma, Arbelt Mgumba ametishia kufuta majina ya wagombea
wa ubunge katika kura za maoni jimbo la Mtera ambao ni Samuel Malecella na Livingstone
Lusinde kupitia CCM kutokana na kuendesha kampeni chafu.
Hatua hiyo ilitokana na wagombea wengine ambao wanaomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo, Philip Elieza na Amos Kusaja, kuwa lalamikia wenzao kwa madai ya kuendesha kampeini chafu ambazo zinavunja kanuni.
Mlalamikiwa mkubwa ni mbunge wa sasa Livingstone Lusinde ambaye anatuhumiwa kulitumia jina la Mwenyekiti wa CCM Taifa na rais Jakaya Kikwete kwa madai kuwa anawasiliana naye mara kwa mara hivyo hawezi kukatwa jina lake hata kama atavunja kanuni.
Mbali na kujigamba kwa hatua hiyo amekuwa akiwatumia vijana kwa kuwanunulia pombe kwa lengo la kufanya fujo katika mikutano mbalimbali.
Hata hivyo Lusinde amekuwa akipata upinzania mzito pale ambapo amekuwa akizomewa katika mikutano mbalimbali katika kata ya Chinugulu, Mpwayungu,Uzi na Nghambaku.
Kutokana na hali hiyo wagombea hao walilazimika kususia mwendelezo wa mikutano kwa madai kwamba uongozi wa mkoa ili utoe ufafanuzi juu ya uvunjwaji wa kanuni ambao unaendelea katika kampeni hizo.
Baada ya wagombea hao kupeleka kesi hiyo kwa Katibu wa CCM, Mugumba alitishia kuwafuta kukata majina yao kutokana na vitendo vyao ambavyo vinavuruga kanuni na taratibu wa kura za maoni.
Hata hivyo kauli ya Lusinde ya kudai kwamba hakuna mtu wa kuweza kukata jina lake kutokana na kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja Mwenyekiti wa CCM Taifa Jakaya Kikwete.
Kutokana na kauli hiyo Mgumba amesema anao uwezo wa kuondoa jina lake katika kura za maoni huku hata kana ana mawasiliano ya moja kwa moja na Mwenyekiti wa CCM taifa.
Hata hivyo Mgumba na alimwagiza Msimamizi wa uchaguzi Uchaguzi, Mathiasi Lusano, kuhakikisha anafuatilia mienendo ya Lusinde na Malecella ambao wanaonekana kuwa kinara wa kuendesha kampeini chafu.
Wanaofanyiwa fujo zaidi katika mikutano ya kura za maoni na Lusinde na Malecella ni Philipo Elieza na Amos Kusaja.
Wakati huo huo katika jimbo la Kongwa Mbunge wa Sasa Job Ndugai,anakabiliwa na upinzania mkubwa ndani ya chama na nje ya chama.
Ndugai anashambuliwa na wapiga kura kwa kushindwa kupeleka maendeleo katika jimbo hilo kutokana na kupeleka maendeleo jimboni hapo.
Wakati Ndugai akijieleza katika mikutano hiyo amekuwa kikumbana na upinzania wakutaka aeleze ni kitu gani amekifanya ndani ya miaka 15.
Hata hivyo Ndugai amekuwa akieleza kuwa ameweza kujenga kipande cha lami chenye urefu wa kilometa tatu na nusu jambo ambalo linaonesha kuwachefua wananchi.
Source: Mwanahalisi.

No comments :

Post a Comment