Australia. Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) ya Heshima ya Sheria (Degree of Doctors of Laws honoriscausa – honorarary LLD) katika Chuo
Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imeeleza kuwa Rais Kikwete anatarajia kutunukiwa shahada hiyo Jumatano wiki hii.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Kikwete atatunukiwa shahada hiyo kwa kutambua uongozi wake uliotukuka, mchango wake wa kuleta maendeleo Tanzania, Afrika na jitihada zake za kuleta amani.
Chuo Kikuu cha Newcastle ni moja ya vyuo vinavyotoa nafasi za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania, chini ya sera ya miaka mingi ya nchi ya Australia kusaidia elimu Tanzania.
Wanafunzi 26 wa Tanzania tayari wamemaliza masomo katika chuo hicho na kurejea nyumbani katika maeneo ya madini, elimu ya juu, vyombo vya habari, masuala ya fedha na masuala ya Serikali.
Wanafunzi 45 bado wanaendelea na masomo katika chuo hicho.
Rais Kikwete na ujumbe wake wataondoka Australia asubuhi ya Julai 30 kurejea nyumbani.
No comments :
Post a Comment