Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Rugemalila Rutatina amejitokeza na kutangaza nia yake ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CCM katika jimbo la Kibaha mjini.
Akizungumza katika ukumbi ya Country side uliopo kibaha mjini jana Rutatina amesema ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo kutokana na kuona hakuna msukomo wowote wa maendeleo kwa muda mrefu katika jimbo hilo hivyo akipata fursa ya kuwa mbunge atashirikiana bega kwa bega ili kuweza kuleta maendeleo na sio vinginevyo.
Alisema kitu kingine kikubwa kilichoweza kumsukuma na kuona vijana wengi wanaoshi katika eneo hilo hawana ajira jivyo wamekuwa wakipata shida kubwa katika kupata fedha amabzo zitaweza kuwasaidia kujiendeleza katika shughuli zao mbali mbali za ujasilimali.
Ametaja vipaumbele vyake kuwa ni ajira kwa vijana wa kibaha kupitia fursa mbali mbali zilizopo, kuimarisha miundombinu ya baarabara pamoja na kujenga stendi ya kisasa pamoja na soko.
No comments :
Post a Comment