Wednesday, August 5, 2015

MNYIKA ASHINDA


Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), ameshinda katika kura za maoni za kugombea ubunge katika Jimbo la Kibamba kwa kupata kura 65 kati ya kura 80 zilizopigwa (asilimia 65).

Katibu wa Jimbo la Ubungo wa Chadema, Justine Malel, alilieleza NIPASHE jana kuwa nafasi hiyo iliwaniwa na wagombea nane ambao waliambulia asilimia 15 huku Mnyika akiongoza.

“Uchaguzi ulifanyika jana (juzi), Mnyika ameshinda kwa kishindo dhidi ya wagombea wenzake nane, pia katika kura za ndani ya chama ameshinda bila ya kupingwa kwa asilimia 100, kwa maana hiyo Chadema tumemsimamisha Mnyika kugombea jimbo la Kibamba,” alisema Malel. 

Mnyika atachuana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenela Mukangara, mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo akitarajiwa kujulikana Jumamosi.

No comments :

Post a Comment