Friday, July 31, 2015

Kunani vyuo vikuu vya Afrika Mashariki ?

                           
Vyuo vikuu vya Afrika Kusini ndio bora zaidi na maarufu barani Afrika.
Katika utafiti uliofanyika majuzi, vyuo vikuu vya Afrika Kusini vilishika nafasi 6 katika orodha ya vyuo vikuu kumi bora.
Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda kimeorodheshwa katika nafasi ya tatu. Chuo kikuu cha Port Harcourt kilichoko Nigeria kimeorodhesha katika nafasi ya sita.
Chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya kimeorodheshwa katika nafasi ya nane.
Jarida la ''The Times Higher Education'' lilitumia idadi na ubora nukuu kutoka kwa wasomi wake. Je viwango vya ubora wa masomo na utafiti wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki vimeshuka ?
Orodha kamili.
1. Chuo kikuu cha Cape Town - Afrika Kusini
2. Chuo kikuu cha Witwatersrand - Afrika Kusini
3. Chuo kikuu cha Makerere - Uganda
4. Chuo kikuu cha Stellenbosch - Afrika Kusini
5. Chuo kikuu cha KwaZulu-Natal - Afrika Kusini
6. Chuo kikuu cha Port Harcourt - Nigeria
7. Chuo kikuu cha Western Cape - Afrika Kusini
8. Chuo kikuu cha Nairobi - Kenya
9. Chuo kikuu cha Johannesburg - Afrika Kusini
10. Chuo kikuu cha Cadi Ayyad - Morocco
Chanzo: BBC Swahili

No comments :

Post a Comment